Na Neema Mtuka Nkasi
Rukwa :Mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali amekabidhi hati za pongezi kwa kata tatu ambazo zimefanikiwa kutekeleza vyema hafua za lishe.
Kata hizo ambazo ni Majengo,Isale na Myula zimefanya vizuri katika eneo hilo la lishe na kutekeleza vyema mpango wa serikali katika kuhakikisha tunaondoa changamoto ya udumavu.
Pia mkuu huyo wa wilaya amesisitiza suala la upatikanaji wa chakula shuleni na kubwa ni kuona kila shule inakua na maeneo makubwa kwa ajili ya kilimo ambapo shule zenyewe ziweze kuzalisha chakula.
“Natamani kuona kila shule inalima na kuzalisha chakula kwa wingi na suala hilo lipo ndani ya uwezo wenu fanyeni kazi kwa kushirikiana ili wanafunzi wapate chakula shuleni ” amesema lijualikali.
Lijualikali amedai kuwa shule kuzalisha chakula ni kitu kinachowezekana na kuwa Kama dhamira ya dhati itakuwepo basi watoto watapata chakula shuleni na kuondoka na tatizo la udumavu ambalo ni aibu wakati ardhi ya kuzalisha chakula ipo .
Afisa lishe wa wilaya hiyo Theresia Matoke kwa upande wake amedai kuwa chakula shuleni kina nafasi kubwa ya kuwafanya Watoto wakawa na afya njema ikiwa Ni pamoja na kufanya vizuri katika masomo yao.
Kikao hicho leo kimeondoka na maadhimio kadhaa katika kuona mkakati wa lishe shuleni unafanikiwa kwa kiwango kinachotakiwa.