NAIBU Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Profesa Peter Msofe,akizungumza na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kutembelea makao makuu ya Baraza hilo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Na.Mwandishi Wetu
NAIBU Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Profesa Peter Msofe, amepongeza utendaji kazi na uwajibikaji wa watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mazingira nchini.
Prof.Msofe ametoa pongezi hizo alipotembelea makao makuu ya Baraza hilo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kushika wadhifa huo.
“NEMC pamoja na changamoto mnazokabiliana nazo, bado mmepiga hatua kubwa katika usimamizi wa mazingira. Mnafanya kazi inayotambulika na kuonekana na wananchi. Endeleeni kujituma kwa ajili ya maslahi ya Taifa, huku mkilinda afya zenu dhidi ya mazingira hatarishi,” amesema Prof. Msofe.
Aidha Prof. Msofe amesisitiza maeneo matano ya msingi kwa watumishi wa NEMC ili kuboresha zaidi utekelezaji wa majukumu yao.
Ametaja Maeneo hayo ni kuweka uwiano kati ya vihatarishi binafsi na vya mazingira ya kazi,Kujifunza na kushirikishana maarifa ya kitaalamu,Kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu,Kuwa wabunifu katika masuala ya mazingira pamoja na Kufanya kazi kwa kuendana na mahitaji ya dunia ya sasa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, ameeleza kuwa Baraza hilo bado linakumbana na changamoto ya kutokuwa na mamlaka kamili ya utekelezaji wa baadhi ya majukumu.
“Tunaendelea na mchakato wa kulifanya Baraza kuwa mamlaka kamili ya mazingira. Kwa sasa, tunategemea vyombo vya ulinzi na usalama katika kutekeleza baadhi ya kazi kutokana na kukosekana kwa sheria inayotoa mamlaka hiyo kwa NEMC,” amesema Dkt. Semesi.