Na Munir Shemweta, WANMM
Ujumbe kutoka nchini Msumbiji umetembelea Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala yanaohusu sekta ya ardhi.
Ujumbe huo wa watu tisa ukiongozwa na Mkurugenzi anayehusika na masuala ya Ardhi na Mipango Maalum wa Wizara ya Kilimo, Mazingira na Uvuvi nchini Msumbiji (MAAP) Bw. Aderito Wetela umetembelea Wizara ya Ardhi tarehe 30 Julai 2025 katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Ukiwa katika ziara hiyo, ujumbe huo uliweza kubadilishana uzoefu na kupata fursa ya kupata maelezo ya namna Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inavyoendesha shughuli zake kutoka kwa Kamishna wa Ardhi Nchini Bw. Nathaniel Methew Nhonge pamoja na wakuu wa idara za wizara hiyo.
Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe huo Bw. Aderito Wetela alieleza namna idara inayohusika na masuala ya ardhi na mipango maalum inavyofanya kazi katika maeneo mbalimbali hususan eneo la ardhi kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.