………
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Kishiri Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wameelezea namna walivyoumia baada ya jina la mgombea udiwani katika kata hiyo Lucas Mpilipili kukatwa.
Wanananchi hao wameeleza kuwa walitarajia jina la mgombea huyo lirudi ili aweze kuwaletea maendeleo katika kata hiyo kwani utendaji kazi wake wameuona tangu akiwahudumia kwa nafasi ya mwenyekiti wa mtaa.
“Tunamasikitiko makubwa sana ndugu yetu kukatwa jina ni mtu ambae tunamtegemea sana katika kuleta mabadiliko chanya kwenye kata yetu”, wameeleza.
Mwisho waliiomba maamlaka husika iweze kuliangalia suala hilo kwaukaribu zaidi ikiwezekana hata kulirudisha jina hilo ili aweze kuwatumikia vyema