NA DENIS MLOWE,MAFINGA
MTIA nia wa Ubunge Jimbo la Mafinga Mjini, Aggrey Tonga amejinadi mbele ya wajumbe huku akiweka vipaumbele endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo kuteka hisia za wajumbe waliowengi.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa kata ya Wambi ,Tonga ambaye ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa aliyepumzika kwa muda alisema katika suala la
Ajira kwa upande wa vijana atahakikisha anawawekea misingi iliyo bora katika sekta za kilimo, viwanda na ujasiriamali.
Alisema kuwa endapo watampa nafasi ya kuwa mbunge atawasemea vijana katika changamoto za ajira wanazokabiliana nazo na kuwaongoza na kuonyesha njia ya kupata ajira.
“Sitafuti nafasi, nataka maendeleo nagombea kwa sababu ya dhamira, si maslahi binafsi na kusisitiza kwa nini halmashauri yenye mapato makubwa bado inakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya maji na barabara” Alisema
Tonga alisema kuwq Wawekezaji wapo wengi, lakini jamii inanufaika kiasi gani ni lazima vijana wapate ajira zenye staha, na wawekezaji wazingatie sheria za kazi.
Aliahidi ubunifu katika kilimo cha mazao mapya yanayokubali Mafinga, ujenzi wa kituo cha afya kipya, na uongozi shirikishi utakaowapa wananchi nafasi ya kumsahihisha pale inapobidi.
Alisema kuwa Ukitaka mali unaipata shambani tunapaswa kufanya kilimo kwa ajili ya biashara mfano kuanzisha vyama vya ushirika, kuwahusisha nao kwa kufanya mazao ya biashara.
Alisema kuwa mjijni Mafinga kuna viwanda mbalimbali hvyo muhimu kuwapigania vijana kuajiriwa na kuwa na mikataba yenye manufaa kwao.
Aliongeza kuwa upande wa sfya tunahitaji kituo Wambi nje ya kile cha jeshi ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii.
Aliongeza kuwa wananchi wanahitaji maji katika kata hiyo kwani hawastahili kukosa huduma hiyo hivyo endapo watampa ridhaa atahakikisha anapambana wapate maji.


