
Watia nia wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Arusha Mjini Arusha, Julai 31, 2025 wameendelea kujinadi mbele ya wajumbe wa chama, katika vikao vinavyoendelea kwa kasi.
Miongoni mwa waliojitokeza ni Paul Makonda, aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye alizungumza mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Sokoni 1.
Makonda alisema: “Nimeacha kazi ili mnipatie kazi. Naomba kazi ninayoifahamu, ninayoipenda, na ninayoimudu. Siombi kazi ya majaribio.”
Alisisitiza kuwa ana imani wajumbe wanamfahamu vyema kutokana na historia ya utendaji wake, na kwamba anakuja na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Arusha Mjini.
Kipaumbele chake: Makonda aliahidi kwamba akipewa ridhaa ya kuwa Mbunge: Ataboresha miundombinu ya barabara, ambayo alisema imekuwa kero kubwa kwa wananchi,
Atashughulikia kero zinazowakabili wakazi kwa mbinu za kitaalamu na kwa kutumia uwezo alionao wa kushawishi maendeleo.