
Mkulima wa Mazao ya Bustani kutoka mkoani Manyara, Bw. Shaban Manota atakuwa Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa mifumo miwili bunifu ya kiteknolojia katika Kilimo, uzinduzi utakaofanyikia katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo 88 Jijini Dodoma.
Tofauti na ilivyozoeleka kwa muda mrefu kuwa wageni rasmi wanakuwa watu wenye ushawishi, Kampuni ya Mazao Hub imeamua kumtumia Mkulima huyo ambaye kwa muda mfupi amepata mafanikio makubwa.
Mifumo anayozindua mmoja ni Mfumo Jumuishi wa Kilimo na mwengine ni Mfumo Jumuishi wa Mazao ya Kilimo iitwayo MazaoHub na CropSupply.com.
Uzinduzi huu unafanyika ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza kwa Maonesho haya ambapo mifumo hiyo inazinduliwa wakati ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaleta mabadiliko kwenue Sekta ya Kilimo ambayo imekuwa ni ya kubahatisha.
Akizungumzi kwa undani uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Mazao Hub, Geophrey Tenganamba anasema kuwa kwa miaka mingi wakulima wamekuwa wakilima bila kumbukumbu, wakifanya maamuzi ya pembejeo bila msaada wa kitaalamu, na wakikumbwa na hasara kubwa baada ya mavuno kutokana na kukosekana kwa mifumo madhubuti.
“Kupitia mifumo ya MazaoHub wakulima, maafisa ugani, wauzaji wa pembejeo (agrovets), wasindikaji, taasisi za fedha na serikali wanashirikiana kwa karibu” anasema Tenganamba.
Afya ya udongo, maendeleo ya mazao, na utendaji wa pembejeo zote zinafuatiliwa – hakuna tena kubahatisha.
Kupitia taarifa za muda halisi na msaada wa karibu kutoka kwa wataalamu wa ndani, wakulima hupunguza gharama, huongeza mavuno, na hupata masoko pamoja na huduma za kifedha. Agrovets, maafisa ugani, wasindikaji na taasisi zote hunufaika kupitia takwimu zilizothibitishwa na uratibu shirikishi.
Hii ndiyo Tech and Touch kilimo kinachoendeshwa kwa takwimu na kuungwa mkono na wataalamu wa eneo husika.
Tunajivunia mafanikio haya chini ya mpango wa Building a Better Tomorrow (BBT) kupitia mradi wa ICT in Agriculture, kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, na Wizara ya Kilimo chini ya Waziri Hussein Bashe.