……….
NA DENIS MLOWE, MAFINGA
BAADHI ya wananchi katika ya Mdahuro jimbo la Mufindi Kaskazini wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kuchagua mgombea ambaye atawaisaidia kuondokana na changamoto zinazowakabili mara kwa mara.
Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya vijana waliozungumza na mwandishi wa habari hizi wakati kampeni za watia nia katika ngazi ya ubunge wa jimbo hilo kuwa ule wakati wa kuwachagua viongozi wasiokuwa na maono na kutatua changamoto za jamii waache.
Walisema kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia changamoto za barabara kama ahadi halafu wakipigiwa kura na kuwa wabunge wanatokomea Dar es salaam na kuwaacha wananchi bila msaada wowote wa utatuzi wa ahadi walizotoa.
Mmoja ya vijana hao Adrian Kiponda wa Mdaburo aliwaasa wajumbe kuhakikisha wanaleta mgombea anayehitajika na jamii ya Mufindi Kaskazini kwani wengi waliopita hawakujali kabisa ahadi walizotoa.
Aidha alisema kuwa ili Mufindi iweze kuendelea kuwa imara lazima wajumbe hao waweze kuchagua viongozi bora watakaoweza kuisaidia wananchi na wanaishi katika mazingira haya kuliko wale wanaokimbilia nje ya wilaya au jimbo.
Aliongeza kuwa ifike wakati wajumbe watuletee mgombea ambaye ana uwezo wa kifedha ambaye hana tamaa za utajiri mara baada ya kuchaguliwa kwani mtu sahihi ni yule mwenye uwezo na anaishi kwenye jimbo letu tangu awali na mgombea kama Luqman Merhab sahihi sana kwa sasa.
Mwananchi mwingine aliyejitambulisha Emmanuel Kipemba aliwaasa wajumbe watoa rushwa ambao wakishachaguliwa wanafikiria namna ya kurudisha hela zao hivyo watuletee kijana mwenye nguvu na uwezo wa kutuletea maendeleo katika jimbo letu.
Katika kampeni hizo mgombea Luqman Merhab amekuwa akiongelewa kwamba ni mtu sahihi katika jimbo hilo hivyo wajumbe wasikosee katika kuhakikisha wanamchagua kuwa mgombea wa ubunge kutokana na kujipambanua kuwa mtu sahihi na anaishi katika jimbo hilo tangu kuzaliwa kwake.
Kwa upande wake mgombea Luqman Melabu aliahidi kushughulikia sekta za barabara, afya na pembejeo, akitumia taswira ya kauli yake ya kumuua panya nyumbani usiangalie rangi ya paka bali angalia paka anayeweza kukamata panya kama mfano wa kumaliza changamoto zinazoikabili Mufindi Kaskazini.
Alisema katika kutatua changamoto yeye sio mtu wa maneno ni mtu wa vitendo zaidi hivyo wajumbe wampe kura ashirikiane na serikali na jamii katika kukabiliana na changamoto hizo kuitatua.