
Gina Huynh, aliyewahi kuwa mpenzi wa Diddy, sasa ametajwa kama Mhusika Namba 3 katika mashitaka ya shirikisho dhidi ya msanii huyo maarufu wa hip hop.
Katika hatua ya kushangaza, Gina ameandika barua kwa jaji akiunga mkono ombi la Diddy la kupewa dhamana ili asubiri hukumu akiwa nje ya gereza.
Katika nyaraka hizo zilizopatikana na TMZ, Gina anaeleza kuwa amemfahamu Diddy kwa miaka mingi na anamchukulia kama baba, mtu wa karibu wa familia, na mfanyabiashara mwenye malengo — si mhalifu kama anavyodaiwa.
Ingawa anakiri kulikuwa na changamoto katika uhusiano wao, anasisitiza kuwa Diddy alikuwa mtu anayejifunza kutokana na makosa yake, na kila mara alipokosea alijitahidi kurekebisha. Anaeleza kuwa kufikia mwisho wa uhusiano wao, Diddy alikuwa amebadilika sana akawa na upendo, uvumilivu na upole, tofauti kabisa na tabia yake ya zamani.