
DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kumpangia kituo cha kazi Balozi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 3,2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na kupangiwa kituo ni kama ifuatavyo:-
(i) Dkt. Khatibu Malimi Kazungu ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Kazungu alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati;
(ii) Prof. Ulingeta Obadia Mbamba ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kwa kipindi cha pili;
(iii) Prof. Aurelia Kokuletage Ngirwa Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kipindi cha pili;
(iv) Balozi Luteni Jenerali Mstaafu Charles Lawrence Makakala ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mzinga; na
(v) Balozi Anderson Gukwi Mutatembwa amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amevunja Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).