Katibu Mkuu wizara ya katiba sheria utumishi na utawala bora Zanzibar Mansoura Mossi Kasim akifungua mafunzo hayo.jijini Arusha leo.
Mkuu wa chuo na Mtendaji Mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania Dkt. Ernest Maboresho akizungumza katika mafunzo hayo jijini Arusha leo.
………
Happy Lazaro, Arusha .
VIONGOZI waandamizi wa sekta ya umma barani Afrika kutoka nchi 9 za kiafrika wamekutana jijini Arusha kwa siku tano kwenye programu ya mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Afrika ambayo yamelenga kuwapa ujuzi, mbinu za ubunifu na ushirikiano za kuwawezesha kuongoza mabadiliko chanya katika utawala, kuimarisha taasisi, kukuza uwajibikaji, na kuchochea ustawi wa mataifa yao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Arusha mgenirasmi Katibu Mkuu wizara ya katiba sheria utumishi na utawala bora Zanzibar Mansoura Mossi Kasim amesema kuwa ,mafunzo hayo kwa viongozi yanajikita katika kubadilisha ule mtazamo wa kuwa wewe kiongozi ni nani.
Aidha Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa viongozi wa sekta ya umma barani Afrika yanaendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya Chandler kutoka Singapore (CIG), kwa kushirikiana na Chama cha Utawala wa Umma na Uongozi Barani Afrika ( AAPAM) chini ya uenyeji wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC).
Ameongeza kuwa,mafunzo hayo yanawakutanisha viongozi takribani 30 wa sekta mbali mbali za Umma kutoka nchi 9 za kiafrika zikijumuisha; Tanzania, Zambia, South Africa, Somalia, Tunisia, Kenya, Lesotho, Uganda, na Malawi.
Ameongeza kuwa ,mara nyingi tumekuwa tukichukulia kiongozi ukishakuwa na teknikal capacity wewe ni kiongozi lakini uongozi una zaidi ya hivyo kuna uongozi wa mabadiliko kwamba unapokuwa kiongozi lazima ulete mabadiliko katika taasisi.
“mafunzo haya yanawaelekeza viongozi kuwa unapokuwa kiongozi lazima ulete mabadiliko katika taasisi, uwe na uongozi wenye maadili ,na wenye mtazamo wa kupeleka mbele maendeleo ambayo yanajikita katika kugusa wananchi na kuleta athari katika maisha ya wananchi .”amesema .
Ameongeza kuwa, mafunzo hayo yatawasaidia kwani kwa sasa hivi Tanzania wapo katika mageuzi makubwa ya sekta ya umma ambayo yanajikita zaidi katika kuchochea uwajibikaji wa viongozi na kuleta matokeo chanya katika taaaisi .
“haya mafunzo yatazidi kuongeza uelewa zaidi kwa kujifunza kutoka nchi tofauti na watazidi kujenga mageuzi ya agenda yao katika utumishi wa umma iwe vipi na ni mkutano ambao utawasaidia katika kuendeleza haya mageuzi ya sekta ya utumishi wa umma ambayo sasa hivi nchi yetu inaendesha.”amesema .
Kwa upande wake Mkuu wa chuo na Mtendaji Mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania Dkt. Ernest Mabonesho amesema kuwa, kauli mbiu ya mafunzo hayo ni “uelewa na usimamizi wa Taifa imara ambapo kauli.mbiu hiyo imelenga kuhakikisha kuwa katika mafunzo hayo washiriki wote wanapotoka waweze kusimamia Taifa imara ,Taifa ambalo watu wake wapo imara kwa maana ya kuwa ni watu ambao wanapata taarifa sahihi wanashirikishwa kwenye mambo mbalimbali ambapo pia viongozi wao wanauwezo wa kuwashirikisha na pia wana uwezo wa kutengeneza sera ambazo zinaweza zikawafaidisha wananchi .
“Sisi kama chuo.cha utumishi wa umma tumepewa majukumu ya kusimamia watumishi wa umma kupitia mafunzo mbalimbali ambapo wanatoa mafunzo kwa watumishi wa umma na ili tuweze kutoa mafunzo vizuri imebidi pia tuhudhurie mafunzo haya ili tuwe na nguvu ya kuweza kutengeneza Taifa imara kwa hiyo tunahitaji ili kuwa na Taifa imara lazima tuwe na viongozi walio imara katika ujenzi wa Miundombinu ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma stahiki kwa wakati na zile ambazo wanazihitaji .”amesema
Ameongeza kuwa ,mafunzo hayo yana hatua kuu tatu ambazo ni kufanya mafunzo hayo ana kwa ana ,baada ya hapo watakuwa na mafunzo ya online pia,na baada ya hapo watakuwa Singapore kwa ajili.ya kwenda kubadilishana mawazo pia namna ya jinsi ya kuendesha serikali au nchi ambayo ni imara katika kuangalia huduma za kijamii kwani huduma za kijamii zikiwa na nguvu tunapata Taifa ambalo ni imara na huduma za kijamii zikiwa legalege tunapata Taifa lililo legelege pia
Naye Makamu wa rais (AAPAM) Ayoub Kilabuka amesema kuwa , chama hicho kinajihusisha na kuwajenga uwezo watalamu katika utumishi wa umma kufanya mafunzo,mikutano na kushiriki midahalo mbalimbali.
Amesema kuwa lengo la kukutana ni katika kushiriki mafunzo maalumu kwa minajili ya kuwajengea uwezo wataalamu viongozi wa kiafrika katika kujenga mataifa imara ya Afrika .
Programu hii inawezesha viongozi kupata mafunzi kuwajengea uwezo ili waweze kujenga taasisi imara katika nchi zao barani Afrika ambapo kwa mwaka huu mafunzo haya yanafanyika mkoani Arusha.
Amesema kuwa,mafunzo haya lengo lake kuu ni kujenga mataifa imara ya Afrika ambapo mataifa imara yanajengwa na taasisi imara na taasisi imara zinajengwa na watumishi imara na watumishi imara wanapatikana kwa kupeta mafunzo na maarifa na kujengewa uwezo katika nyanja mbalimbali za kiakili maarifa kiuchumi na kisiasa.
Ambapo lengo kubwa ni kuwajengea uwezo na kuwa na viongozi imara ambao watakwenda kuboresha taasisi zao na baadaye kukuza mataifa yao kuwa imara zaidi na kuweza kujitegemea kiuchumi kisiasa na kijamii.
Katika mafunzo haya, mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wabobezi kutoka barani Afrika na Singapore, zikiwemo uelewa wa dhana ya mataifa imara, dhana ya uongozi unaozingatia mabadiliko, uwajibikaji katika sekta ya umma, ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa kiuchumi, mapitio Mipango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), pamoja na maono na mikakati ya muda mrefu katika kuifikia Afrika bora ijayo.