
YANGA SC mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26 hawapoi kutokana na kasi yao kwenye utambulisho wa wachezaji wapya.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Yanga SC ilitwaa taji la Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC likiwa ni taji lao la 31. Baada ya mechi 30 walikusanya jumla ya pointi 82 na safu ya ushambuliaji ilifunga jumla ya mabao 83.
Ni Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota mwenye miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Staa huyo ana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi kwa wengine.
Licha ya kumtambulisha rasmi Agosti 3 2025 usiku, imeelezwa kuwa Yanga tayari walimalizana na Doumbia tangu mwezi Mei mwaka huu. Doumbia anakuja kurithi mikoba ya Stephanie Aziz Ki. Hii ni kutokana na akili, nguvu na uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani zikiwemo 8 na 10 akiwa uwanjani.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.