Afisa Kilimo Bodi ya Pamba Tanzania akionesha namna Wanavyotumia ndege nyuki na trekita katika kunyunyuzia dawa kwenye mashamba
………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza.
Bodi ya Pamba Tanzania imeendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima ikiwa ni pamoja na kuongeza matrekita 300 kwa msimu huu ili mkulima aweze kulima eneo kubwa kwa muda mfupi.
Hayo yamebainishwa Leo Jumatatu Agosti 04, 2025 na Afisa Kilimo wa Bodi hiyo, Sharifa Salumu wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Wakulima Nane Nane,ambapo kwa Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza.
Amesema kwa msimu uliopita walikuwa na matrekita 400 ambayo yamemlimia mkulima wa pamba kwa hekari moja kwa shilingi elfu 35 ,bei hiyo ni pungufu ukilinganisha na matrekita binafsi ambayo yanalimiwa kwa elfu 60 kwa hekari.
Aidha, ameeleza kuwa endapo mkulima akilima kwakutumia mbegu ya UKM08 kwa wakati na kwanafasi ya sentimita 60 kwa 60 mstari hadi mstari na sentimita 30 kwa 30 kutoka shimo hadi shimo mkulima huyo atakuwa na uwezo wa kupata kuanzia kilo 1000 hadi 1200.
“Tunawashauri wakulima walime kwakufuata utaratibu ili waweze kuona mnyororo wa thamani wa zao la Pamba,tunavifaa vya kisasa kwaajili ya upuliziaji wa mashamba na tunamisimu miwili tunatumia ndege nyuki ambayo inapuliza kwenye mashamba ya wakulima” Amesema Salumu.
Akizungumzia soko la Pamba kwa Kanda ya Ziwa na mikoa mingine inayolima pamba amesema ni zuri kwani wakulima wanalima pamba na wanunuzi wananunua tangu msimu ulivyofunguliwa Mei 02, 2025.
“Bei iliyokuwa elekezi ya Serikali ilikuwa ni 1,150 lakini kwa sasa mkulima ananunuliwa pamba kwa shilingi 1200 hivyo soko la pamba liko vizuri”,