Johannesburg, Afrika ya Kusini & Dar es Salaam, Tanzania — Mapenzi hayajui mipaka,na katika ushirikiano wao wa kwanza kabisa, mwimbaji wa Afrika Kusini Cici na nyota wa Tanzania Mimi Mars wamefanya ukweli huu kuwa hai katika wimbo wao mpya wa
kupendeza wa “Running”, ulioangaziwa kwenye album ya Cici ya hivi karibuni, iitwayo Busisiwe 2.0.
Running (kukimbia) ni utunzi wenye hisia ambao unasimulia hadithi ya roho mbili
zinazokimbiliana, kila mmoja akivutwa na mapenzi, kuponywa kwa uhusiano, na
kuunganishwa na hatima. Pamoja na maelewano ya kiuchangamfu na nyimbo za kihisia, Cici na Mimi Mars wametengeneza simulizi hii ya kimapenzi ambayo inawagusa wote wawili kwa karibu, na ulimwengu wote.
“Ni wimbo kuhusu kuchagua mpenzi, kuhusu kuacha hofu na kukumbatia uwezekano wa kitu kizuri,” Cici anasema. “Kufanya kazi na Mimi kulileta usawa kamili wa ulaini na nguvu ambayo hadithi hii ilihitaji,”.
Mimi Mars anaongeza, “kuna kitu cha kipekee kuhusu wimbo huu. Unazungumzia aina ya upendo ambao sisi sote tunaota, aina ambayo haukimbii, bali unakimbilia.”
Kama kivutio kwenye album ya Busisiwe 2.0, Running inajipambanua kwa usimulizi wake mahiri wa hadithi, tamaduni mbalimbali na ushirikiano wenye nguvu kati ya sauti mbili zinazopendwa zaidi barani Afrika. Ushirikiano huo sio tu unaunganisha sauti za Kusini na Mashariki ya bara la Afrika, bali pia unasherehekea kwa pamoja uthubutu wa wanawake wa kuweza kupambana na changamoto wanazozipitia.
Wimbo huo kwa sasa unapatikana kwenye majukwaa yote muhimu ya usambazaji muziki, na tayari umeanza kugusa mioyo na kuwavutia wasikilizaji kote barani Afrika.
Kwa mahojiano, kuweka booking, au fursa za matangazo, tafadhali wasiliana na:
The House of Thom
Baruapepe: info@houseofthom.com
Instagram: @thehouseofthom
Simu: +27 60 8278 460