DAR ES SALAAM
Culture and Development East Africa (CDEA) kwa kushirikiana na Tamasha, Tuzo za Filamu pamoja Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wameandaa maonyesho ya Mashariki Creative Economy Expo 2025 ambapo yatawakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya ubunifu.
Akizungumza na wanahabari leo Agosti 5,2025 jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu CDEA, Ayeta Wangusa amesema kuwa maonyesho hayo yatafanyika siku tatu jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mlimani City ambapo wadau kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Rwanda, Uganda na wenyeji wao Tanzania.
Amesema kuwa, katika siku hizo tatu kutakua na Matukio muhimu ambayo yatakua yanaendelea ikiwemo uzinduzi rasmi wa maonyesho ya bidhaa za ubunifu, Majadiliano ya kifedha na biashara ya utamaduni na Mkutano wa jioni Samaki Samaki.
“Siku ya pili kutakua na mazungumzo kuhusu uchumi wa Muziki, mafunzo ya ubunifu, Muziki, Filamu,mitindo Uandishi, uzinduzi wa ripoti ya UNESCO Afrika Book Industry, kikao cha uwelewa COSOTA na usiku wa shot ambapo utafanyika Nafasi Art Space”
Ameongeza”siku ya mwisho ya maonyesho hayo kutakua na mjadala wa sera za Filamu licha ya kuwa Tanzania hakuna sera tutatumia ya Afrika Mashariki, muendelezo wa mafunzo ya ubunifu, fashion show pamoja vyumba maalum ambapo wafanyabiashara kwenye sekta Filam watakutana na kubadilishana uzoefu na kujifunza mambo mbalimbali kwenye ubunifu.”
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sanaa za Ufundi Basata ,Bona Masenge amesema kwamba wamepokea mradi huo kwa furaha kubwa kwani utakuwa msaada kwa wabunifu kujitangaza kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha ameeleza kwamba kwa sasa kamati maalum ya Kitaifa itakayohusisha wadau mbalimbali imeshaanza vikao ili kuhakikisha taratibu zote zinazohitajia zinakamilika na pia amewataka wadau na wasanii wachangamkie fursa hii kwa kujisajili ili kushiriki maonesho hayo.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Bodi ya Filamu, Emmanuel Ndumukwa amesema kwamba hii ni fursa kwa wasanii kujifunza na kutumia nafasi hiyo kubadilisha uzoefu kutoka kwa wasanii wengi na jinsi ya kutumia mafunzo hayo kutumia nafasi za matumizi sahihi ya motandao ya kijamii ili kujipatia fedha.