
MKALI wa kucheka na nyavu ndani ya kikosi cha Simba SC, Steven Mukwala inaelezwa kuwa huenda akauzwa na kutokuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu wa 2025/26.
Mukwala yupo na Simba SC kambini nchini Misri ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya. Taarifa zinaeleza kuwa RS Berkane inawania saini ya mshambuliaji huyo anayefanya kazi na Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids.
Rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa 2024/25 mshambuliaji huyo alifunga jumla ya mabao 13 kwenye mechi 26 alizocheza akitmia dakika 1,094 huku mguu wake wakulia ukifunga mabao mengi ambayo ni 10 mguu wa kushoto mabao mawili na kwa pigo la kichwa bao moja.