Mgombea wa udiwani Kata ya Kunduchi, jijini Dar es Salaam anayetetea nafasi yake Michael Urio ameibuka kinara katika kura za maoni kwa kuwabwaga wagombea wengine wa wanne kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa matokeo ya kura za maoni yaliyotangazwa na msimamizi wa Kata hiyo Agosti 4, 2025- Urio ameongoza kwa kupata kura 257, anayefuatia Joyce Haule kura 250, Emmanuel Mkuchu hura 240, Hashemi Komba kura 30 na Happyness Juustin alipata kura 12.
Urio ambaye ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, awali jina lake halikurudi wakati wa uteuzi lakini baadaye alirejeshwa.