Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB, Wakili Patrick Kipangula akimkabidhi Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Clifford Ndimbo, kwa niaba ya Maafisa Habari na Wasemaji wa Sekta ya Michezo nchini baada ya kukidhi vigezo vya Kisheria na kuthibitishwa.
Bodi imeendelea kutoa vitambulisho hivyo kwa Waandishi, Wahariri, Maafisa Habari, Watangazaji wa Radio na Televisheni, Wapiga Picha, wawakilishi na Waandishi wa Kujitegemea waliokidhi vigezo.