Neema ametoa wito huo katika Maenesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini ambapo wataalamu kutoka VETA wameweka banda kuelimisha umma kuhusu shughuli za VETA, mafunzo ya ufudi na stadi zinazotolewa na VETA Kanda ya Kusini.
“Nawaasa wananchi wa Mtwara na Lindi na Mikoa ya pembezoni na vijana walioko mtaani wamemaliza masomo hawana aiira, waje kwenye Vyuo vyetu vya VETA kuna vitu vingi wanaweza kujifunza ili kupata ujuzi (Skills) stadi za kazi ya mikono ambazo zitawasaidia kujiajiri au kupata ajira na kujipatia kipato,” amesema.
Neema amesema Vyuo Vya VETA vinatoa mafunzo ya ufundi stadi katika sekta mbalimbali kama vile ujenzi, uchomaleaji na kadhalika kwa wahitaji wakiwemo waajiri walio na nafasi na wenye uhitaji wa kuongeza ujuzi.
“Napenda kuwaasa wananchi , vijana waliomaliza shule ,chuo, na hawana ajira waje VETA ndio suluhisho la ajira pekee,” amesema na kuongeza kuwa VETA inatoa mafunzo ya muda wa wiki moja mpaka miaka mitatu.
Katika hatua nyingine, Neema amesema serikali inajenga vyuo vipya vitano vya VETA katika Mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuimarisha na kuendeleza mafunzo ya ufundi stadi Mikoa ya Mtwara na Lindi na mikoa ya pembezoni kama vile Songea.
“Ujenzi wa Vyuo hivyo vitano vinaendelea katika Wilaya ya Nachingwea , Kilwa na Liwale Mkoani Lindi, Nanyumbu na Tandahimba Mkoani Mtwara,” amesema na kuongeza kuwa ujenzi wa Vyuo hivyo utakamilika mapema mwaka na kutoa nafasi ya watu kujiunga na kupata ujuzi na stadi za kazi ya mikono.
Kwa sasa Kanda ya Kusini Mashariki Ina Vyuo vitano tu vya VETA. “Baada ya ujenzi kukamilika tutakuwa na Vyuo kumi Kanda ya Kusini Mashariki,” amesema.