Na Mwandishi Wetu
Jumla ya Tanzania wapatao 10,000, wameweza kupatiwa matibabu bure, katika Kambi ya siku tatu ya upimaji wa afya na macho yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mwisho mwa wiki hii Jijini Dar es Salaam.
Akitoa taarifa ya mwisho mara baada ya mwisho wa Kambi hiyo Alhaji Mohammedraza Dewji, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia ithninasher Mkoa wa Dar es Salaam alisema kuwa majumuisho ya mafunzo hayo ya Imam Hussein (as), kwa mwaka huu yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuvuka malengo.
Kwa mujibu wa Alhaji Mohammedraza, alisema Kambi hiyo ni kumbukizi ya kifo cha Mjumkuu wa Mtume Muhammad (SAW) Imam Hussein (as), iligawanyika Katika sehemu kuu mbili, moja ilikuwa kupata elimu juu ya Imam Hussein (as) na nyingine ni utolewaji bure wa vipimo vya afya, Dawa na kufanyiwa opeesheni ya macho
Aidha, Alhadji Mohammedraza alisema kuwa Katika utolewaji wa elimu juu ya Imam Hussein (as), wakazi hao walielezwa hali halisi ya Kiongozi huyo, ambaye aliutoa uhai wake kwa ajili ya kupigania umma wa babu yake na alitaka uwepo wa usawa, haki, huruma na imani kwa wote bila ya kujali Dini, Kabila, jinsia au kipato.
Mwenyekiti, huyo alisema kuwa mafanikio yaliyopatikana Katika mafunzo hayo ya afya mwaka huu, ni tofauti na mwaka Jana kutokana awamu hii kuwa na mwitikio mkubwa wa watu wengi kujitokeza katika kupata huduma na matibabu.
Pia, akielezea mafanikio yaliyopatikana mwaka huu mbali na kupata elimu, pia walielezwa jinsi ya kujizuia na upatikanaji wa magonjwa ya macho, ikiwemo kutokutumia vitu vyenye mwanga mkali, kufikicha macho wakati yakiwa na vumbi pamoja na kutotumia miwani ya macho bila ya ushauri wa wataalam.
Alhaji Mohammedraza alisema kuwa zaidi ya watu 4800 walijitokeza katika upimaji wa macho katika idadi hiyo, kuna wagonjwa wengine 289 walikutwa na changamoto za mtoto wa jicho na matatizo mengine ambao watapangiwa siku ya kwenda kufanyiwa upasuaji.
“wapo waliokutwa na ugonjwa wa mtoto wa jicho wapatao 97 na walipelekwa kwenye Hospital ya Medwell iliyopo Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na wengine waliobakia, watapangiwa siku zingine ya kwenda kupata matibabu na upasuaji”, alisema mwenyekiti huyo.
Aidha, mwenyekiti huyo alisema kuwa wapo wagonjwa wengine waliojitokeza katika Kambi hiyo, hawakuwa tayari kwenda kupatiwa huduma katika hospitali ya Jumuiya iliyopo Kibaha kutokana na umbali, lakini watapangiwa kwenda kupata huduma katika hospitali yao nyingine iliyopo Temeke Charitable Hospital bila gharama yoyote.
Pia, alisema kuwa wagonjwa 2,817 walipewa miwani ya kusomea na wengine wapatao 1813 waliopewa miwani ya kutembelea huku 3500 waliopewa dawa na kutibiwa matatizo ya macho.
Vile vile, Alhaji Mohammedraza, aliendelea kueleza kuwa katika Kambi hiyo ya siku tatu pia walikusanya jumla ya Chupa za Damu salama 229 kwa kushiriiana na mpango wa Taifa wa Damu salama, ambapo malengo ya ukuanyaji huo wameelekeza Damu hizo zipelekwe kwenye hospitali zenye uhitaji.
Alhaji Mohammedraza alisema kuwa wakina mama zaidi ya 427 walifanyiwa vipimo vya kansa ya shingo ya kizazi, ambapo 181 kati ya wakina mama 17, walitakiwa kuonana na daktari kwa vipimo zaidi.
Aliendelea kueleza kuwa wakina mama 12 miongoni mwao walitibiwa pale pale uwanjani na kuruhusiwa kurudi makwao na wengine 12, waliopima kansa ya matiti waligundulika kuwa na matatizo na kuhitaji ukaribu wa madaktari.
Hata hivyo, kwa upande wa kina baba mwenyekiti huyo alisema kuwa kulikuwa na vipimo vya tezi dume na kati ya waliopima 6 waligundulika kuwa na ishara ya tezi dume pamoja magonjwa yasioambukiza, ikiwemo pressure na sukari na ugonjwa uliosahaulika wa Afya ya akili watu 4800 walipatiwa elimu juu ya ugonjwa huo ambao umeanza kushamiri.
Aidha Mwenyekiti huyo alitoa rai kwa taasisi na mashirika mengine yenye uwezo kuweza kutoa huduma za afya kwani kwenye mafunzo hayo watu waliofika na kupatiwa huduma na baada kupimwa na kukutwa na maradhi bila ya kujua nini kinachomsumbua na kuitaka jamii kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara pindi wakipata fursa ya kufanya ivyo.
Kwa upande wake Daktari mkuu Daktari Alhussein Molloo akiongelea juu ya Kambi hiyo ya siku 3 alisema kuwa magonjwa mengi ni magonjwa ya macho na yale yasioambukiza, 77 waliona madaktari 236 walifanyiwa vipimo vya ultrasound 88 walitambuliwa kwa ufuatiliaji wa muda mrefu na upasuaji mkubwa .
Dk, Molloo alisema kuwa baada ya kuwapima na kujua hali za afya zao na kuwapatia elimu jinsi ya kuishi na kujua afya zao na kupima afya na watu hawajui jinsi ya kupata matibabu.
Aidha, Dk matatizo yote ya uvimbe yatapasuliwa Katika hospitali za Jumuiya hizo za Ebrahim Hajj KSIJ Charitable Eye Center na tutawafatilia maendeleo yao.
Kwa upande wake, mratibu wa Kambi hiyo Jameel Kassam, alisema kuwa wamejifunza kutoka kwa Imam Hussain (as) kuwa hudumia binadamu ni kufanya ibada.
Mratibu huyo alisema kuwa kwa siku tatu, jina moja lilisikika kila kona ya Mnazi Mmoja ni Imamu Hussein (as) kama ihara ya kuenzi kujitoa kwake kwa ajili ya kupigania haki na usawa kwa jamii na kuwahudumia bila ya kujali dini, kabila, jinsia na rangi yake bali kunahitajika usawa na kutoa matumaini, heshima, na elimu.
Alisema kuwa Mafunzo ya Imam Hussain ni kielelezo cha imani inayotekelezwa kwa vitendo.
Akiongelea juu ya Kambi hiyo, Sachi Hassan Kajogoo ambaye ni mmoja ya watu waliojitokeza Katika Kambi hiyo, alisema kuwa alifurahishwa na mpangilio mzima wa mafunzo hayo kuanzia kwenye kuingia na utaratibu wa kupewa elimu juu ya Imam Hussein (as) na kutambua kuwa Imam Hussein (as) alijitoa kwa wanyonge.
Kajogoo alisema kuwa utaratibu wa kupata matibabu ulikuwa nzuri mno kuanzia kwenye upimaji wa macho hadi kwenye kuchangia Damu.
“Alikuwa akiumwa na kichwa mara kwa mara na macho yalikuwa yanatoa machozi hadi aliposikia kupitia vyombo vya habari kuna taasisi inatoa huduma za upimaji wa afya bure aliamua kwenda kupatiwa huduma hizo ambapo amepimwa na kujulishwa kuwa miwani aliyokuwa akivaa iIikuwa lenzi yake ni tofauti na uono wa macho yake pamoja na kupatiwa miwani mingine ya kutembelea nay a kusomea pamoja na kupewa dawa” alisema Kajogoo.
Naye mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Zogowale iliyopo wilani Kibaha ajulikanae kwa jina la Aisha Mohammed, ambaye alisema kuwa alikuwa na changamoto ya macho yalikuwa yanatoka machozi na uono hafifu kwa mbali hususani akiwa darasani.
Alisema kuwa baada ya kupimwa macho yameonekana kuwa tatizo kubwa ni vumbi hali iliyopelekea kujifikicha fikicha mara kwa mara na kutokea maumivu kwenye macho yake na kupatiwa dawa na miwani.