Mratibu wa masoko wa kampuni hiyo Tanzania,Awadh Maftah akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye maonesho ya nanenane Njiro

Mratibu wa masoko wa kampuni hiyo Tanzania,Awadh Maftah akionyesha moja ya mitambo inayopatikana katika kampuni hiyo kwenye maonesho hayo jijini Arusha.



Happy Lazaro, Arusha
KAMPUNI ya Sola ya Sunking inayotengeneza bidhaa za Sola ambazo ni taa za Sola, pamoja na mitambo ya Sola kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwenye biashara imekuja na mitambo yenye uwezo wa kufanya kazi kwenye mahoteli makubwa pamoja na kwenye mahema ya utalii katika maeneo ya porini.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mratibu wa masoko wa kampuni hiyo Tanzania,Awadh Maftah wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro.
Amesema kuwa, wamefikia hatua ya kuja na mitambo hiyo mikubwa kutokana na mahitaji ya soko kwenye katika mahoteli pamoja na kwenye mahema hususani porini ambapo hakuna umeme wanakuwa na mahitaji makubwa ,hivyo ni wakati.wao.sasa kuchangamkia fursa hiyo .
“Msimu huu wa nanenane tumeleta bidhaa mbili za Sola kwa ajili ya wateja wetu na endapo umeme ukikatika una uwezo mkubwa wa kuendelea na shughuli zao ambapo bidhaa hizo ni Power Play Pro ambapo ni mtambo wenye uwezo wa kuchaji simu,TV,vifaa vidogo vya umeme pamoja na Laptop. “amesema .
Aidha ametaja mitambo mwingine kuwa ni Power Hub ambao una uwezo wa kuendesha Friji ,taa za umeme bila kuwepo kwa wearing yoyote na kuwezesha kuendesha vifaa vyote vya nyumbani bila wasiwasi wowote.
Awadh amefafanua kuwa ,kwa upande wa mtambo wa Power Hub una uwezo wa betri ya 2.5 KW ,Pure sine wave Inverter 3.3 KW pamoja na Palel mbili za 450 W kila mmoja ambapo aliwataka kupiga simu no 0800781023 kwa ajili ya kupata huduma mahali popote pale walipo.
Awadh ametaja aina ya mitambo ya Sunking kuwa ni pamoja na Boom Pro,Home plus pro,Home plus,Power Play Pro,pamoja na Hub na kwenye msimu huu wa nanenane wanapatikana katika mikoa ya Dodoma ,Arusha,Mbeya,Mwanza ,Morogoro,pamoja na Lindi ,hivyo amewataka wananchi katika msimu huu kuchangamkia fursa hiyo kwa ajili ya kupata huduma hizo zenye uhakika na guarantee ya miaka miwili.
Aidha amefafanua kuwa, bidhaa hizo pia zinapatikana kwa mkopo ambapo mteja ana weza kukopa na kulipa kidogo kidogo kwa muda wa miaka miwili hadi mitatu kulingana na makubaliano ya mtambo waliochukua na hii ni ili kuwawezesha wananchi wote kuweza kunufaika na kuondokana na changamoto mbalimbali .
“Kampuni yetu tunapatikana nchi nzima na tuna mawakala mikoa yote ya Tanzania na tupo Unguja na Pemba pia , na utofauti wetu na wengine ni kuwa Sola zetu sisi ni bei nafuu na zina ubora wa kiwango cha juu na mteja ana uwezo wa kulipia kidogo kidogo kuanzia shs 350 kwa siku na anaweza kupatiwa taa ya Sola”amesema Awadh .
Awadh amesema kuwa, wameweza pia kusambaa hadi maeneo ya vijijini ambapo wanatoa huduma hiyo ya Sola ambapo mawakala wamesambaa kila mahali lengo likiwa ni kuhakikisha mwananchi popote pale alipo anapata huduma hiyo kwa uhakika na kwa wakati muafaka.
Aidha aliwataka wananchi katika maeneo mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo kwa kuzitumia bidhaa zao ambazo ni za uhakika na za bei nafuu na zinadumu kwa muda mrefu sana.