Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema kwasasa Ushirika umeimarika kwakuwa na Mifumo ya kisasa ya kidigitali ambayo inachangia uwazi katika utendaji wa Vyama vya Ushirika.
Mhe. Senyamule amebainisha hayo Agosti 6, 2025 wakati akitembelea mabanda mbalimbali ya Vyama vya Ushirika katika kijiji cha Ushirika kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane Jijini Dodoma.
“Nilipotembelea mabanda nimefurahishwa sana kuona Ushirika upo kidigitali, hii itawawezesha wanaushirika kuwa sehemu ya Usimamizi kwakuwa taarifa za Vyama zitapatikana kwa uwazi na haraka,” amesema Mhe. Senyamule.
Aidha, amepongeza Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC) pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kuandaa Kijiji cha Ushirika na kuwaleta wanaushirika pamoja .