
Aliyewahi kuwa Spika na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma
Tarehe ya Kuzaliwa: Januari 21, 1963
Elimu ya Msingi:
Mheshimiwa alianza safari yake ya elimu katika Shule ya Msingi Mtare kuanzia mwaka 1971 hadi 1977.
Elimu ya Sekondari:
Aliendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Kibaha kati ya 1978 hadi 1981, kisha akaendelea na elimu ya sekondari ya juu katika Shule ya Sekondari Old Moshi kati ya 1982 hadi 1984.
Elimu ya Juu:
Mnamo mwaka 1986 hadi 1988, alipata Stashahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Mweka. Baadaye aliendelea na Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyoipata kati ya 1989 hadi 1993.
Mwaka 1994 hadi 1995, alisoma Masomo ya Uzamili (Post Graduate) katika Chuo cha Kilimo nchini Norway, na baadaye akahitimu Shahada ya Umahiri (Masters) kutoka chuo hicho hicho mwaka 1995 hadi 1996.
Safari yake ya kielimu iliendelea tena katika Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI), ambako alisoma na kupata Shahada ya Umahiri katika Usimamizi wa Biashara (MBA) kati ya 2005 hadi 2008.
Uongozi wa Kisiasa:
Mheshimiwa amekuwa Mbunge wa Jimbo la Kongwa kwa kipindi cha miaka 25, akihudumu kwa uaminifu mkubwa na mchango wake katika maendeleo ya jimbo hilo na taifa kwa ujumla umetambuliwa na kuheshimiwa.