

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.
Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Majaliwa ameandika:
“Ninaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa salamu za pole kufuatia msiba wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Yustino Ndugai.
“Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape utulivu Familia, Wana Kongwa, Familia yote ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wana CCM wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.”