Mratibu wa masoko TAHA ,Dkt. Steven Tumaini akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya nanenane katika viwanja vya Themi Njiro.

Mratibu wa masoko TAHA ,Dkt. Steven Tumaini akitoa elimu kwa mmoja wa wakulima kuhusu kilimo cha nyanya baada ya kutembelea banda la TAHA kwenye maonesho hayo mkoani Arusha.


………..
Happy Lazaro, Arusha
Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa ya kilimo.cha mbogamboga na matunda kwani kilimo ni biashara na ni ajira na kinalisha watu wengi hivyo wametakiwa kuungana ili waweze kupata kipato na kuwa na afya bora .
Hayo wamesemwa jijini Arusha na Mratibu wa masoko TAHA ,Dkt. Steven Tumaini wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya nanenane katika viwanja vya Themi Njiro.
Amesema kuwa, kumekuwepo na fursa nyingi sana kwenye kilimo na wengi wamepata mwamko wa kulima kilimo.hicho ambacho kina manufaa makubwa sana kwa wananchi na jamii kwa ujumla kutokana na kuwepo kwa telnolojia mbalimbali za kisasa zinazotumika.katika kilimo hicho .
Aidha amesema kuwa, mwitikio wa vijana ni mkubwa hususani wale waliohitimu vyuo ambao wameingia kwenye kilimo wakiwa wapya ambapo changamoto kubwa inayowakabili vijana ni kutojua mazao gani waingie nayo kwenye biashara kwani kilimo sasa hivi ni biashara lazima tuanzie sokoni tushuke hivyo elimu wanayoipata hapa ni kuhusu mazao gani ili waweze kuingiza mtaji waweze kusonga mbele .
“Changamoto kubwa sasa hivi ni magonjwa ila tuna wataalamu kutoka taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuwafundisha vijana kujua ni mitego gani watumie pamoja na dawa kwa ajili ya export na kujua ni fursa gani zilizopo kwenye kilimo.”amesema Dkt Steven .
Ameongeza kuwa, kwa mwaka wa 20 sasa wapo kwenye sekta ya mboga mboga na wanahudumia mikoa 26 lakini nanenane ndio sehemu rafiki ya kuweza kukutana na na wawekezaji wakulima na wasafishaji .
Dkt.Steven amesema kuwa mazao ambayo wanayatangaza mwaka huu kwenye mboga mboga ni parachichi,ndizi ,kitunguu,nyanya,na viazi pamoja na mazao mengine ya mboga mboga .
Amesema kuwa , kwa mwaka huu wanaonyesha teknolojia ya kibanda mwendo kwamba wale wanaotafuta ajira sasa ndo wakati wake kwamba vijana wale ambao hawawezi kulima lakini wanaweza kuongeza thamani wanaweza kutumia teknolojia ya kibanda mwendo kwa ajili ya kujiajiri .
Amefafanua kuwa ,mbali na kibanda mwendo pia tuna teknolojia ya umwagiliaji kwa njia ya matone pamoja na green house ambapo wamekuja na uwekezaji kwa ajili ya kuongeza thamani kwenye mazao mbalimbali ikiwemo lishe kutoka kwenye mazao mbalimbali .
Amesema kuwa ,kipekee zaidi kwa mwaka huu wana wadau kuanzia wauza mbegu,wauza miche, na wote ambao wanahitaji drip irrigation ,au green house ,trekta,wote wapo ndani ya nanenane .
“Tumejipanga kwani tupo Zanzibari, Arusha a Dodoma ambapo huko kote kuna wawalilishi wetu lakini hapa mwaka huu wameshafikisha watu zaidi ya Mia nane kwa Arusha peke yake na wana malengo ya kufikisha watu zaidi ya elfu moja na sio wakulima wadogo tu lakini pia kuna wasafirishaji ,wauza mbegu,na wanaotaka kuwekeza katika nchi hii “amesema .
Ameongeza kuwa, zao kuu mwaka huu ni parachichi na limeshawabeba kwani limefanya vizuri sana na kuna watu wanawauzia parachichi, viatilifu kwa ajili ya kutibu,pamoja na vifungashio kama makreti na vingine vingi kwa ajili ya kuhudumia mteja ikiwemo maboksi kwa ajili ya kusafirishia parachichi kwenda Ulaya pamoja na nchi nyingine jirani.
“Tunawakaribisha sana wananchi kufika katika banda letu kwa ajili ya kupata mafunzo na kupata wateja kwa ajili ya kununua mazao yao na kupata fursa ya kuonana na wataalamu wa kilimo wa Taha ambao wapo katika vibando mbalimbali kwani wamejiunga na wadau mbalimbali.kwa ajili ya kuonyesha mbegu zao pamoja na kuhudumia wananchi ili waweze kupata huduma ya kilimo, biashara pamoja kuongeza thamani ili kupunguza upotevu wa mazao Tanzania. “amesema Steven.
Aidha amesema kuwa, mwitikio wa vijana ni mkubwa hususani wale waliohitimu.vyuo ambao wameingia kwenye kilimo wakiwa wapya ambapo changamoto kubwa inayowakabili vijana ni kutojua mazao gani waingie nayo kwenye biashara kwani kilimo sasa hivi ni biashara lazima tuanzie sokoni tushuke hivyo elimu wanayoipata hapa ni kuhusu mazao gani ili waweze kuingiza mtaji waweze kusonga mbele .
Steven amefafanua kuwa,wanatoa pia elimu ya wao kuwa wanachama na kujiunga kwenye vikundi ili waweze kumudu na kujua kilimo ni biashara sasa hivi .
Amefafanua kuwa, baada ya kuwapa elimu hiyo wamekuwa wakiwafuatilia kwa kumpigia kila mmoja baada ya hapa kujua aliyaonaje maonesho ili wajue alichojifunza na huduma gani anaitaka .
Aidha amewataka wananchi kufika kwenye banda lao kwa ajili ya kujionea teknolojia mbalimbali na kuweza kubadilisha mtazamo wao na kuweza kuwekeza kwenye kilimo kwani kilimo sasa sio mateso bali kimekuwa na teknolojia ambayo inawavutia hata ambao wasipenda kulima wanalima kwani sasa hivi kilimo ni biashara kwa maendeleo.
Kwa upande wa kijana aliyetembelea banda hilo ,Marko Sabuni amesema kuwa kwa.kufika.kwenye banda hilo la Taha ameweza kubadilisha mtazamo wa kilimo baada ya kujionea fursa mbalimbali.zilizopo kwenye kilimo.cha mboga mboga pamoja na teknolojia za kisasa zinazotumika .
Aidha amewataka vijana kutembelea kwa wingi banda la Taha na kuweza kubadilisha mtazamo wao kwani kilimo ni ajira na ni biashara hivyo wafike wapate elimu mbalimbali namna ya kulima kisasa.
Sarah Benard amesema kuwa, anashukuru Taha kwa kuweza kumbadilishia mtazamo akiwa kama.kijana kwa kuweza kujiajiri kwenye maswala ya unga wa lishe unaotokana na mboga huku akiwataka vija wengine kuwekeza kwenye kilimo.cha mboga mboga kwani kinalipa sana.