Makamu wa Rais Afrika Mashariki jumuiya ya wataalamu wa utawala wa umma barani Afrika ,Ayoub Kilabuka wakati akizungumza katika.ufungaji wa mafunzo maalumu ya programu ya mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Afrika

Mkurugenzi wa mafunzo kwa watumishi wa umma Chuo cha utumishi wa umma Tanzania ,Sijali Korojelo aliyemwakilisha Mkuu wa chuo hicho na Mtendaji Mkuu Dokta Ernest Mabonesho akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa Taasisi ya uongozi ya Chandler Singapore ,Ho Wei Jiang akizungumza katika ufungaji wa mafunzo hayo jijini Arusha .
Na Happy Lazaro, Arusha
Nchi za Afrika pamoja na viongozi na watumishi wa umma wametakiwa kuendelea kujengewa uwezo kupitia mafunzo mbalimbali ya uongozi ili kuongeza tija, ufanisi na kuimarisha taasisi za umma katika nchi zao.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wataalamu wa Utawala wa Umma Afrika Mashariki (AAPAM), Ayoub Kilabuka, wakati wa kufunga mafunzo maalum ya uongozi kwa viongozi wa sekta ya umma barani Afrika, yaliyofanyika kwa siku tano jijini Arusha.
Amesema kuwa ,mafunzo ni nguzo imara sana kwa maendeleo ya kila mtumishi kwani mabadiliko ya teknolojia, kiuchumi na kisiasa yanahitaji elimu na utambuzi ili yaweze kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika taasisi zao .
Amesema kuwa ,mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo viongozi kutoka taasisi za umma barani Afrika na yanalenga hasa kuwajengea uimara katika kufanya uamuzi na kujenga taasisi imara na mataifa yao imara .
“mafunzo hayo yamekuwa ya mafanikio sana kwani washiriki wamepata kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa maadiliko kwa teknolojia na katika uendeshaji wa serikali pamoja na mabadiliko katika nyanja za kimataifa na ushirikiano ambapo kubwa zaidi umeelezwa kuhusu namna ya kupambana na magonjwa au tahadhari ya afya ya akili kwa watumishi na wafanyakazi wa serikali.”amesema Kilabuka .
“leo tuna furaha kubwa kuhitimisha mafunzo haya na kupeleka ujumbe kwa taasisi zingine za Afika kuendelea kuwajengea uwezo viongozi wao ili kuweza kuwa na mataifa ambayo hapo imara katika nyanja za kiuchumi,kijamii na kisiasa pamoja na kuwa na viongozi ambao ni waadilifu na ambao wanqeza kuleta matokeo chanya kwa maendeleo ya nchi zao na Afrika kwa ujumla.”amesema .
Kilabuka amefafanua kuwa,malengo ya mkutano huu ni kuwajengea uwezo viongozi wa Afrika ambao wanatoka katika ofisi za umma au watumishi wa serikali kutoka nchi mbalimbali barani Afrika .
“Mafunzo haya yalijumuisha viongozi kutoka nchi 11 barani Afrika na lengo hasa ni kuwajengea uwezo ili kuwa viongozi imara ambao watakuja kuchangia maendelea ya taasisi zao kuwa imara na baadaye nchi zao kuwa imara .”amesema Kilabuka.
Ameongeza kuwa ni matarajio yao kuwa wamepata tija katika mafunzo hayo na wataenda kuleta mabadiliko chanya ambayo yatasaidia kukuza uimara wa taasisi zao na nchi zao kwa ujumla .
Aidha Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa viongozi wa sekta ya umma barani Afrika yaliendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya Chandler kutoka Singapore (CIG), kwa kushirikiana na Chama cha Utawala wa Umma na Uongozi Barani Afrika ( AAPAM) chini ya uenyeji wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC).
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mafunzo kwa watumishi wa umma Chuo cha utumishi wa umma Tanzania ,Sijali Korojelo aliyemwakilisha Mkuu wa chuo hicho na Mtendaji Mkuu Dokta Ernest Mabonesho amesema kuwa, katika mafunzo haya ya uongozi kwa ajili ya viongozi wa Afrika kupitia programu ya chuo cha utumishi wa umma wameshiriki katika maswala mbalimbali ikiwemo kutoa baadhi ya wakufunzi ambao wameendesha mada katika magunzo hayo .
Korojelo amesema kuwa, wameweza kuungwa na mfumo wa E government ya Tanzania ambayo imewapitisha namna gani serikali ya Tanzania inatumia mifumo katika kuimarisha uendeshaji wa shughuli za serikali .
Ameongeza kuwa, mafunzo haya yanalenga kujenga taasisi imara au nchi imara za kiafrika ambapo viongozi hawa wengi wao ni wafanya maamuzi katika nchi zao kwa hiyo kwa mafunzo haya na ujuzi ambao wameupata na watakaporudi katika nchi zao watashiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha kwamba wanahamasisha habari za sera ,mabadiliko katika kuhakikisha kwamba tunafikia mataifa ambayo yanakuwa imara zaidi .
“Chuo cha utumishi wa umma pia baada ya kukamilisha mafunzo hayo moja ambavyo washiriki walifanya ni kwenda kwenye safari za kujifunza katika jumuiya ya afrika mashariki pamoja na chuo cha Esami .”amesema Korojelo.
Aidha amesema kuwa chuo cha utumishi wa umma Tanzania chini ya kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kina uwezo na kina nyenzo na vifaa kuhakikisha ya kwamba inaweza kuratibu shughuli yoyote kubwa kama hiyo na wapo tayari pale watakapohitajika kupata shughuli yoyote ambao inahitaji uratibu wa namna hiyo na amewakaribisha wote wenye shughuli kama.hizo wawaone katika.chuo cha utumishi wa umma na wao watapanga shuguli zao vizuri na wataratibu katika viwango vya kimataifa.
Naye Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu katika chuo cha ufundi Arusha ,Emmanuel Ishika amesema kuwa ,wamejifunza kwenye programu hiyo kuwa mataifa yanainuka na baadhi ya mataifa mengine yanaanguka kutokana na uongozi ama uongozi bora .
“Tumeweza kujifunza namna gani mataifa yanainuka na yanakuwa imara ambapo tumefahamu kuwa Tanzania ni moja ya mataifa imara sana na ni baada ya kulinganisha na mataifa mengine kama Tunisia,Zimbabwe,Kenya, Mauritius, tukajua kutokana na jinsi tunavyotenda kazi na jinsi tunavyojiimarisha kwenye uongozi nchini kwetu Tanzania ni moja ya mataifa imara .”amesema Emmanuel .
Ameongeza kuwa ,baada ya hapa wataenda Singapore kwa ajili ya kujifunza ni namna gani Singapore imeweza kuwa Taifa imara hasa katika kutoka kwenye dunia ya tatu mpaka kwenda kwenye dunia ya kwanza na sisi nchi yetu kama Tanzania uchumi wetu unaimarika kutoka kwenye uchumi wa kati na kwenda uchumi wa kiwango cha juu na programu hii ni ya maana sana .