
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi sabini na tatu (73) kama ilivyoainishwa katika hili tangazo.
MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA HESABU) – NAFASI 55
1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kushiriki katika kuainisha maeneo yanayoweza kufanyiwa ukaguzi na kutunza taarifa
zake;
ii. Kushiriki kuandaa mpango wa ukaguzi (Audit Programme) kila mwaka;
iii. Kushiriki katika utekelezaji wa mpango wa kazi wa ukaguzi kila mwaka;
iv. Kushiriki kufanya tathmini ya mpango wa kazi na kupendekeza mabadiliko inapobidi
kulingana na tathmini ya taarifa ya utekelezaji ya mpango wa kazi;
v. Kukagua nyaraka za matumizi, maendeleo, amana, wakala, mifuko, miradi maalum
na mapato ya Serikali;
vi. Kutayarisha hoja na barua za ukaguzi;
vii. Kuhakikisha kuwa hoja na barua za ukaguzi zinatolewa na kushughulikiwa kwa wakati
unaotakiwa; na
viii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazoendana na
sifa na fani yake.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 21 Agosti, 2025
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI