Na Rahma Khamis Maelezo
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe, Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira bora kwa Vikosi vya SMZ ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanya kazi sambamba na miundombinu ambayo itaongeza Ari katika kutekeleza majukumu yao
Ameyasema hayo katika Viwanja wa Chuo Cha Mafunzo Hanyegwa Mchana Wilaya ya Kati katika ufungaji wa Kozi ya Maafisa kwa Vikosi vya Zimamoto na Chuo Cha Mafunzo Zanzibar.
Aidha amewataka wapiganaji hao kutoridhika na hapo na badala yake kuendelea kutafuta taaluma zaidi za kijeshi na elimu ya kiraia ili kuendelea kuwa watendaji wenye elimu bora ambazo zitaleta ufanisi zaidi katika KAZI za kila siku.
Amefahamisha kwamba Afisa yeyote wa Chombo Cha Ulinzi na Usalama ana jukumu la kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Nchi unakuwa imara muda wote hivyo kila mmoja anadhamana ya kuhakikisha Amani inaendelea kudumu.
Mhe Hemed amewataka wapiganaji hao kutunza haki, kujiepusha na rushwa, dharau, majivuno na kiburi katika maisha
Akisoma risala Afisa Msaidizi kutoka Chuo Cha Mafunzo Issa Chuom ameomba kupatiwa Ndege ya bandia kwa ajili ya mafunzo katika Chuo Cha Mafunzo ya Uokozi Kitogani sambamba na kutengenezewa barabara ya lami katika njia za ndani ya Vyuo vyao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe, Masuod Ali Mhammed ameishukuru Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Dk Hussein Mwinyi katika kuleta maendeleo
Akitoa taarifa ya Kozi hiyo Kamishna wa Chuo Cha Mafunzo CP, Khamis Bakari Khamis amesema kuwa jumla ya wapiganaji 154 wamehitimu Kozi ya Uafisa ambapo kati yao 85 kutoka Chuo Cha Mafunzo na 69 kutoka Kikosi cha Zimamoto na Uokozi.
Amefahamisha kuwa mbali ya Kozi ya Uafisa pia wamepatiwa taaluma za ziada ikiwemo usalama wa barabarani, Itifaki na Mahusiano ya Umma.