Songea, Agosti 09, 2025
HESLB imeendelea kutoa elimu kuhusu uombaji na urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Songea za Wavulana na Wasichana zilizopo mkoani Ruvuma.
Wanafunzi wa shule hizo wameeleza kufurahishwa na hatua ya HESLB kuwafikia shuleni na kuwapatia maarifa ya awali kuhusu namna ya kujiandaa vema katika masuala ya uombaji mikopo.
Pamoja na mafunzo ya Ana kwa ana; shule hizo zilikabidhiwa mabango yenye maswali na majibu yanayoulizwa mara kwa mara kuhusiana na mikopo na ruzuku za wanafunzi ambapo zitawezesha kupata uelewa wa zaidi kuhusu masuala ya mikopo.
“Bango hili litakuwa rejea muhimu kwa wanafunzi na walimu, ambapo litakuwa chachu ya kuongeza uelewa na kuwasaidia wanafunzi kujiandaa mapema katika mchakato wa kuomba mikopo na urejeshaji wake baada ya masomo” alisema ndugu Nguwa Florence, Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wao, wanafunzi waliipongeza HESLB kwa jitihada hizo na kuahidi kutumia elimu waliyoipata kwa manufaa ya baadaye.