Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai katika mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Msunjulile, Kongwa Mkoani Dodoma, Agosti 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai katika mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Msunjulile Kongwa, Mkoani Dodoma, Agosti 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai yaliyofanyika katika kijiji cha Msunjulile, Kongwa Mkoani Dodoma, Agosti 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwapa pole familia ya Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai katika mazishi yaliyoanyika katika kijiji cha Msunjulile Kongwa, Mkoani Dodoma, Agosti 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim. Majaliwa akisalimiana na wabunge wastaafu katika mazishi ya Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai yaliyoanyika katika kijiji cha Msunjulile Kongwa, Mkoani Dodoma, Agosti 11, 2025. Kutoka kulia ni aliyekuwa Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali, aliyekuwa Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangwala, na aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwili wa Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ukishushwa kaburini katika mazishi yaliyoanyika katika kijiji cha Msunjulile Kongwa, Mkoani Dodoma, Agosti 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakiwa na baadhi ya viongozi katika mazishi ya Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai yaliyofanyika katika kijiji cha Msunjulile Kongwa, Mkoani Dodoma, Agosti 11, 2025. Kutoka kushoto ni Spika Mstaafu, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (BARA) John Mongella, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Mjane wa Marehemu, Dkt. Fatuma Maganga ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
