Katika hatua muhimu ya kuimarisha ustawi wa kifedha wa watumishi wa umma nchini, Benki ya Exim Tanzania imefanya maboresho kwenye huduma yake ya Wafanyakazi Loan na kuzindua kampeni ya mikopo ya watumishi wa umma maarufu kama ‘Kopa Kiboss’. Exim Tanzania inakuwa benki ya kwanza nchini kumwezesha mtumishi wa umma kufanya marejesho kwa muda wa miaka 11 ambapo anaweza kuchukua kiasi cha mkopo kuanzia Tzs 200,000 hadi Tzs Milioni 200. Benki hiyo, inayoongoza kwa suluhisho za kifedha za kibunifu, inalenga kuwafikia na kuwanufaisha watumishi kote nchini kwa suluhisho zisizo na kifani.
Maboresho haya pia yanatoa fursa ya kipekee ya kuhamisha mikopo (loan takeover) kutoka taasisi nyingine, hivyo kuifanya benki ya Exim Tanzania kuwa taasisi ya kwanza ya kifedha nchini kuwezesha zoezi hili kupitia mfumo bunifu wa mtandaoni wa ‘Employee Self Service’ (ESS) portal unaojulikana kama ‘Utumishi Portal’. Huduma hii ya kisasa imeundwa mahsusi kuwapatia watumishi wa serikali masharti bora ya mikopo, hupatikana kwa haraka, na urahisi usio na kifani, huku tayari watumishi kutoka taasisi mbalimbali wakinufaika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Agnes Kaganda, Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Tanzania, alisisitiza dhamira ya benki: “Lengo letu kuu ni kuhakikisha watumishi wa umma wananufaika na suluhisho za kifedha zinazoleta mabadiliko chanya na ya kweli katika maisha yao. Kwa kuhamisha mikopo yao iliyopo, tunalenga kuwapunguzia mzigo wa madeni na kuwapatia masharti bora ya ulipaji yaliyoboreshwa kulingana na mahitaji yao binafsi ya kifedha.”
Lengo la ‘Wafanyakazi Loan’ ni kumsaidia mtumishi wa umma kutotegemea chanzo kimoja cha kipato, ambayo ni mishahara yao, kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile kuhudumia familia, kulipa madeni, na kufanya biashara ili kujiendeleza kiuchumi. Hivyo, mkopo huu utawapa watumishi suluhisho za kifedha na kuwajengea utulivu wa kifedha na kufungua milango ya fursa mpya.
Naye Mtenya Cheya, Mkuu wa Bidhaa na Uhakika wa Mapato, alifafanua zaidi kuhusu urahisi wa huduma hii, “Tumebuni huduma hii kwa kuzingatia urahisi na uharaka. Waltumishi watakuwa na fursa ya kuongeza mikopo yao kulingana na uhitaji wao. Ulipaji wa mkopo utapangwa kwa mafungu sawa ya kila mwezi (EMI) katika kipindi chote cha mkopo, jambo linaloongeza urahisi na uhakika kwa wakopaji na kuwapa amani ya akili.”
“Pia, mkopo huu unajumuisha bima ya maisha ya mkopo (credit life insurance), kuhakikisha kuwa salio la mkopo linalobaki linalipwa iwapo mkopaji atafariki dunia au kupata ulemavu wa kudumu. Hii inampa amani mtumishi na familia yake huku ikilinda mustakabali wao wa kifedha,” aliongeza Mtenya.
“Hivyo, tukiwa kama taasisi ya kwanza kuongeza muda wa marejesho pamoja na masharti nafuu, tunatoa wito kwa watumishi wote wa umma kote nchini kuchangamkia fursa hii ya kipekee ya ajili ya maendeleo yao, binafsi, familia zao, ama kuanzisha au kukuza biashara zao kama sehemu ya kuongeza kipato chao. Karibuni sana Exim Bank Tanzania,” anamalizia Elihoria Matillya, Meneja Mkuu – Mauzo kutoka Benki ya Exim Tanzania.
Ili kuomba mkopo huu, watumishi wa umma wanaweza kutembelea tovuti ya ESS portal kupitia anwani https://ess.utumishi.go.tz, kisha chagua Benki ya Exim, na kufuata hatua rahisi kukamilisha maombi yao.
Benki ya Exim Tanzania inaendelea kujitolea kuwa mshirika wa kuaminika katika kutoa huduma za kifedha kwa watumishi wa umma, ikiwapatia zana na fursa za kufikia malengo yao na kujenga maisha bora na yenye tija.