
Klabu ya Simba SC imethibitisha kumsajili kiungo kiraka raia wa Guinea, Naby Camara, kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka miwili, utakaomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2027.
Camara mwenye umri wa miaka 23 ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati na beki wa kushoto. Anasajiliwa ili kuongeza nguvu kwenye upande wa kushoto wa ulinzi, nafasi iliyoachwa wazi na Mohammed Hussein Zimbwe Jr, ambaye amejiunga na watani wa jadi, Yanga SC.
Nyota huyo mpya wa Simba SC aliwahi kuichezea klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia na msimu uliopita alikuwa akiitumikia Al-Waab Sporting Club ya nchini Qatar.