Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amewataka wafanyabiashara wa Soko la kimataifa la Kariakoo kuwa mabalozi wa amani ili biashara zifanyike kwa utulivu na usalama kipindi hiki nchi ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu, kauli aliyoitoa leo Agosti 15 ,2025 wakati akifungua tamasha la Gulio la Kariakoo, Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi za umma zinazohusika na usimamizi na uratibu wa wafanyabiashara nchini leo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Gulio la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Agosti 15,2025.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Bw. Yusuph Mwenda amesema wataendelea kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara wa Kariakoo ili walipe kodi kwa uaminifu .
Mratibu wa tamasha la Gulio la Kariakoo (Kariakoo Festival) George Lupenza amesema tamasha hilo litafanyika ndani ya saa 72 kuanzia leo na lengo ikiwa ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara kupata masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.(Habari na Picha na Shirika la Masoko ya Kariakoo)