
NYOTA mpya wa Simba SC, Naby Camara raia wa Guinea tayari ameanza kazi katika kikosi hicho kuelekea msimu wa 2025/26 chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Camara ni beki wa kushoto alitambulishwa rasmi kuwa nyeupe na nyekundu Agosti 14 2025 kuwa mali ya Simba SC kwa kandarasi ya miaka miwili.
Yupo nchini Misri na kikosi cha Simba SC ambacho kimeweka kambi huko kwa maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.