
Katika mkutano na maafisa wake, Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema anakaribisha juhudi za “dhati” za Donald Trump kumaliza vita vya Ukraine. Shirika la habari la Urusi, TASS, linaripoti kuwa Putin alieleza hatua zilizochukuliwa na utawala wa sasa wa Marekani na kusifu juhudi za Washington za kusitisha mapigano na kufikia makubaliano yenye maslahi kwa pande zote zinazohusika.
Putin alisema:
“Kuweka mazingira ya muda mrefu ya amani kati ya nchi zetu, Ulaya na duniani kwa ujumla ni muhimu.”
Kwa upande wa Marekani, White House imetangaza kuwa Trump atatumia njia zote za kidiplomasia kumaliza vita hivi. Waziri wa Wanahabari wa Ikulu, Karoline Leavitt, alisema katika mahojiano na Fox News kuwa mkutano wa kilele kati ya Trump na Putin, utakaofanyika kesho Alaska, utajumuisha:
Leavitt aliongeza kuwa Trump ana njia nyingi anazoweza kutumia na ana matumaini ya kutumia diplomasia na mazungumzo kuleta amani nchini Ukraine, akibainisha kuwa kuna vikwazo na hatua nyingine nyingi zinazoweza kutumika iwapo zitahitajika.