Naibu Kamishna mkuu wa TRA ,Mcha Hassan Mcha ambaye alimwakilisha Kamishna mkuu akifungua mafunzo hayo jijini Arusha
Rais wa Chama cha wahasibu Tanzania , CPA Godvictor Lyimo akizungumza kwenye mafunzo hayo

Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Chama cha Wahasibu Tanzania(TAA) wametoa mafunzo maalumu kwa Taasisi za umma kuhusu sheria ya fedha ya mwaka 2025.
Akifungua mafunzo hayo leo jijini Arusha Naibu Kamishna mkuu wa TRA ,
Mcha Hassan Mcha ambaye alimwakilisha Kamishna mkuu , amesema kuwa wapo kwa ajili ya kutoa elimu kwa chama cha wahasibu Tanzania ambao ni wadau muhimu katika mchakato wa kukusanya mapato ya serikali kwani wana nafasi kubwa ya kufanya na utaalamu wao unasaidia katika kutoa mawazo na ushauri wa kitaalamu ambao unasaidia katika kukusanya na kutoa kodi za serikali .
“Leo tumekuja kwa ajili ya kuwaelimisha maeneo mbalimbali kwani tumeanza mwaka mpya wa fedha ambao unakuwa na mabadiliko mbalimbali ya kisheria hivyo tumekuja kuelimishana mabadiliko hayo yanahusu nini .”amesema Mcha .
Amesema kuwa wahasibu wengi ni kutoka mashirika ya umma, hivyo elimu hiyo itawasaidia wakati wa kufanya miamala mbalimbali waweze kukusanya kodi ya serikali ambazo zipo zimeanzishwa kwa mwaka huu wa fedha wa 2025/2026 .
Amefafanua kuwa, katika hao pia wanapokea mawazo maoni na ushauri ambao utasaidia kuboresha utendaji kazi wao na maeneo ambayo wanahitaji na hata kupokea mawazo kwa ajili ya mwaka ujao au mawazo ambayo yatasaidia kuboresha mwaka mwaka huu wa fedha na njia nzuri ya kukusanya na njia nzuri ya kufanikisha kazi zetu hizo .
Naye Rais wa Chama cha wahasibu Tanzania , CPA Godvictor Lyimo amesema kuwa chama hicho kinashughulika na maslahi mapana ya wahasibu na wakaguzi Tanzania .
“siku ya leo tumeandaa mafunzo maalumu kwa siku mbili ambayo yanakwenda kugusa mashirika ya umma .”amesema CPA Lyimo .
“Kwamba mnavyofahamu kuwa kila mwaka julai 1 tuna mabadiliko ya sheria yanayopitishwa na bunge letu la Jamhuri ya Tanzania na huwa tunakuwa na mabadiliko ya Sheria mbalimbali zinazogusa sekta binafsi pamoja na mashirika ya umma .”amesema .
“Sisi kama chama cha wahasibu na wakaguzi nchini Tanzania tumeona basi ni vyema kuendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ambapo leo tumeanza na mashirika ya umma kutoa elimu.kwamba wao kama mashirika wana wajibu gani katika mabadiliko ya Sheria ili kuweza kuwa sehemu ya mabalozi wa ulipaji kodi wa hiari pasipo kuwa shuruti.”amesema .
“Tutakuwa na mafunzo ya siku mbili na Leo tumebahatika kuwa na ufunguzi wa mafunzo yetu ambayo yamefanywa na naibu kamishna mkuu wa mapato Tanzania.”amesema .
Ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali kwenye eneo la ulipaji kodi ambayo sana ni wigo finyu kwa walipa kodi Tanzania kitu ambacho tunafikiri kwamba kimetokana na elimu duni kwa watanzania walio wengi kwenye swala la ulipaji kodi .
Amefafanua kuwa ,wao kama chama wanaendelea kutoa mafunzo na elimu kwa watanzania wote ili kuwasaidia kujua umuhimu wa wao kuchangia katika pato la Taifa ambapo swala kubwa walilo nalo ni kwamba ni watu wachache sana wanaolipa kodi kitu ambacho kinafanya mazigo wa kodi uwe mkubwa kwa wachache wanaolipa .
“Kwa hiyo kupitia elimu ya mafunzo kama haya tunategemea kwamba wengi wataingia kwenye wigo hata wale ambao wapo kwenye sekta rasmi iliyosajiliwa tunatamani na wao wawe na sehemu yao ya kuchangia hivyo tunatamani mafunzo haya hata baada ya hapa sisi kama.chama tutaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na wa dhati kwa serikali ya awamu ya sita lakini pia kwenye taasisi zetu mbalimbali na mashirika ya umma ,sekta binafsi, na vyama vidogo vidogo vya wafanyabiashara kuendelea kutoa elimu hii ili kuweza kuendelea kuchangia pato kubwa kwenye Taifa letu la Tanzania .”amesema .
Aidha amefafanua kuwa,mbali na elimu kuna swala la watu kuwa na kulinganisha kuwa amelipa kodi ameona kitu gani kwa hiyo tuna swala la elimu ambayo inakwenda kugusa moja kwa moja ni nini chini ya sheria wewe mtanzania wa kawaida ,mfanyabiashara wa kawaida ,shirika la umma la.kawaida ni nini ufanye kuchangia ,lakini pia tuna upande wa Pili wa elimu kuwafanya watanzania wajue kuwa kodi yao wanalipa inafanya nini serikali.inatumia fedha nyingi kwenye huduma za kijamii.ambazo nyingi zinatokana na fedha zinazotokana na kodi kwa hiyo hiyo elimu lazima iweze kufahamika.kwenye jamii ya watanzania ili kila mtu anapokuwa na utayari wa kulipa kodi ajue kwamba analipa lakini anategemea kupata kitu fulani kwa hiyo elimu pande zote mbili ni muhimu na wanaamini kabisa itakuza pato la Taifa kupitia michango kupitia kodi na tozo mbalimbali.
Nao baadhi ya washiriki hao wamesema mafunzo hayo yatasaidia sana kuongeza wigo mpana katika ukusanyaji wa kodi nchini.