*Awataka Vijana kuwa chachu ya kuhakikisha ajenda ya Usalama inakuwa endelevu.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka leo amehitimisha na kufunga mafunzo ya wiki miezi 4 ya askari 114 mkupuo wa 20 wa jeshi la Akiba yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mvumi.
Akizungumza na wahitimu na wananchi waliojitokeza katika sherehe hizo DC Shaka amepongea na kutoa shukrani za dhati kwa JWTZ kupitia Makao Makuu na Kamandi ya Jeshi la Akiba kwa kuratibu mafunzo kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu na kupelekea wilaya hiyo kuongeza idadi ya askari kila mwaka.
“Mshauri Jeshi la Akiba nifikishie Pongezi zangu huko, tunaelewa kuwa Jeshi la Akiba ni nguzo muhimu katika mfumo wa ulinzi wa Taifa letu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua wajibu wa kila raia kulinda uhuru, umoja, na usalama wa nchi yetu” Shaka.
Amewataka Askari hao mafunzo waliyoyapata yasiishie kwenye kuhitimu bali wakayaishi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku katika kuisaidia jamii na nchi hasa wakati wa matukio muhimu na ya msingi ambayo hugusa uzalendo wa kila mmoja.
“Mkiwa uraiani ndeleeni kuwa mfano wa nidhamu, utiifu na uzalendo katika jamii, mnapoitwa kwa majukumu ya taifa, mjitokeze bila kusita, mkiweka mbele maslahi ya nchi kuliko binafsi “
” Muwe mstari wa mbele katika kusaidia kudhibiti majanga, ulinzi na usalama wa raia, na kushirikiana na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama kwa kutambua viashiria vya uhalifu, kuviripoti na kuvidhibiti” Shaka
Aliwakumbusha vijana kuwa Taifa letu liinahitaji wananchi wenye moyo wa kujitoa kama walivyothibitisha wao na kuwa sehemu ya safu muhimu ya ulinzi wa nchi.
“Morogoro na Wilaya ya Kilosa zina nafasi kubwa katika uchumi wa nchi kutokana na kilimo na rasilimali nyingine ambapo usalama ni nguzo ya maendeleo, nendeni mkawe chachu ya kuhakikisha usalama inakuwa ajenda endelevu kwa nchi yetu” Shaka
Hata hivyo DC Shaka amebainisha kuwa Jeshi la Akiba ni chelezo la Taifa lipo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inabaki salama, yenye mshikamano, na yenye maendeleo.
“Hii ndio Tanzania anayoipigania Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wito wangu kwenu nyote muendelee kuwa mabalozi wa amani, mshikamano, na maendeleo katika kila eneo mtakalokuwepo” *Shaka*