Na Editha Karlo,Kigoma
WAANDISHI wa habari wa Mkoa wa Kigoma wamepewa mafunzo usalama na ulinzi wa kimwili ,kidigitali na afya ya akili katika kipindi hiki muhimu cha kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja ambayo yamefanyika katika ofisi za chama cha waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma(KGPC) na kushirikikisha baadhi ya waandishi toka vyombo mbalimbali Mkoani humo Katibu wa chama cha waandishi Mkoa wa Kigoma (KGPC)Mwajabu Hoza amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yamekuja wakati sahihi.
Mkufunzi wa mafunzo ya usalama na ulinzi kwa waandishi wa habari Adela Madyane ambaye pia ni mwandishi wa habari akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi waliohudhuria mafunzo hayo katika ofisi za chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kigoma(KGPC)
“Nina waomba waandishi wenzangu tuzingatie haya mafunzo tutakayofundishwa leo na wakufunzi wetu kwani haya ni mafunzo muhimu kwetu na yamekuja kwa wakati sahihi ambapo tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu”alisema Mwajabu
Katibu Mwajabu alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa”Empowering journalist for infurmed community”unaofadhiliwa na umoja wa ulaya(EU)na shirika la maendeleo la uswisi(SDC).
Mkufunzi Izack Aron akitoa mada ya usalama mitandaoni kwa baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma.
Amesema pia mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa International Media Support(IMS)Union of Tanzania press Club(UTPC)pamoja na jamii Africa.
“Hawa wakufunzi wetu wa leo ni waandishi wenzetu ambao walijengewe uwezo na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)na kisha kutakiwa waje kutujengea uwezo na sisi ili tuwe salama kupitia mafunzo haya watakayotupa leo” Mwajabu aliongeza .
Mwenzeshaji wa mafunzo hayo Adela Madyane ambaye ni mwandishi wa habari akitoa mada ya ulinzi na usalama alisema waandishi wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotekeleza majukumu yao ya kazi kwa kujilinda wakati wote kwani ulinzi na usalama huanzia kwa mwandishi mwenyewe.
Baadhi wa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza mada ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa Mkoa wa Kigoma
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Izack Aron ambaye ni mwandishi wa habari akitoa mada ya usalama mitandaoni amewataka waandishi kuzingatia umuhimu wa kuweka nywila imara katika vifaa vyao vya kazi na kuepuka kubofya viunganishi visivyo salama mitandaoni.
“Tuwe makini tunapotumia mitandao mambo ya kupenda kujiunda wifi za bure tuache utajikuta taarifa zako zinadukuliwa bila wewe kujua,pia tuache tabia ya kubofya viunganishi ovyo vingine vinakuwa siyo salama”