Makamu wa rais wa MCT na mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Fedha na Utawala Ndugu Yusuf Khamis Yusuf, akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Omega Ngole (wa pili kushoto), kutambua mchango wa taasisi yake wakati wa kongamano lililowaleta Mabaraza ya Habari ya Afrika na nje ya Afrika, 14-17 Julai 2025, Jijini Arusha.
Wanaoshuhudia: FCPA Happiness Nkya, mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Ukaguzi wa Hesabu za Fedha (wa kwanza kulia), Jaji mstaafu Robert Makaramba, mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Maadili (wa tatu kulia), na Katibu Mtendaji wa MCT na Katibu Mkuu wa Mabaraza ya Habari Duniani, Ernest Sungura (kushoto).
Tukio hili limefanyika Alhamis, 14 Agosti, 2025, Jijini Dar Es Salaam.