NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala zima la kuboresha sekta ya michezo uongozi wa shule ya sekondari Baobab pamoja na chuo cha afya cha Bihas vilivyopo Kata ya Mapinga Wilaya ya Bagamoyo imeamua kufanya bonanza kubwa la michezo ambalo limeshirkisha jumla ya shule 12 za sekondari lengo ikiwa ni kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi wa kike na wakiume.
Bonanza hilo ambalo limehudhuliwa na viongozi wa serikaali, walimu kutoka shule mbali mbali, wadau wa michezo pamoja na wanafunzi kutoka maeneo mengine ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo washindi katika mchezo wa soka wameweza kuzawadia zawadi mbali mbali ikiwemo kupatiwa vikombe pamoja na medali ikiwa pamoja na wale wanafunzi wa kidato cha sita ambao wamefanya vizuri katika taaluma.
Akizungumza wakati wa halfa ya bonanza hilo Afisa taaluma wa Halmshauri ya Wilay ya Bamoyo Juma Selemani ambaye pia aliyekuwa ni mgeni rasmi katika shughuli hiyo amewapongeza kwa dhati viongozi wa Taasisi ya Baobab kwa kuweza kuamua kukuza na kuibua vipaji vya wanafunzi kupitia bonanza hilo ambalo limeweza kuwa la kihistoria kutokana na mwamko kuwa ni mkubwa.
Amebainisha kwamba katika bonanza hilo ameweza kubaini kuwepo kwa vipaji mbali mbali kutoka kwa wanafunzi wa kike na wakiume katika mchezo wa soka sambaambaa na vipaji na uwezo mkubwa katika mashindano ya kitaaluma ambayo yameweza kuonyeshwa na wanafunzi mbali mbali.
“Napenda kutoa pongezi kubwa kwa uongozi mzim wa taasisi ya Baobab ambaapo leo tumeweza kushuhudia bonanza ili kubwa ambalo limeambatanaa na michezo mbali mbali pamoja na uzinduzi wa chuo cha afya naa sisi kama serikali tutaaendeleaa kushirikiaanaa beg kwa bega kwa lengo la kuwez kuleta maatokeo chaanyaa katika sualaa laa kukuza taalumu pamoja naa kukuza vipaaji kwa wanafunzi,”amebainisha Suleman.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya Baobab Shani Swai amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuendelea kukuza michezo na kwamba watajitahidi sana kuhakikisha wanajenga mazingira rafiki kwa lengo kuwawezesha wanafunzi waweze kucheza viwanjaa vyenye ubora ambao unatakiwa.
Naye Mkuu wa chuo cha afya cha Baobab Nelsen Rahul amebainisha kwamba dhumuni la bonanza hilo ni kuendelea kuwashirikisha watu mbali mbali wakiwemo wanafunzi pamoja na watoto wenye ulemavu kwani michezo na kwamba mikakati yao ni kuendeleza kufanya mabonanza zaidi kwa lengo la kukuza vipaji na kuimarisha afya.
Katika bonanza hilo ambalo limeweza kugonga nyoyo za wanafunzi timu ya shule ya sekondari Shushila wameweza kubuka na mabingwa wa jumla baada ya kuwachapa wapinzani wao wenyeji wa shule ya Sekondari Baobao kwa bao 1-0 katika mchezo mkaali uliokuwa wa vuta ni kuvute kutokana ana wachezaji wote kuonyesha vipaji vya hali ya juu.
Baadhi ya shule za sekondari ambazo zimeweza kupata fursa ya kipekee katikaa kushiriki katika Bonanza hilo ni pamojaa na wenyeji shule y Sekondari Baobab,Dunda Sekondari, Mapinga, Dunda, Nia njema,Kerege, Kingani, Fukayosi.