
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za kupanga njama za kufanya uhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salim Morcase amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika Ukumbi wa Mwitiongo, Maili Moja wilayani Kibaha, wakidaiwa kupanga njama za kutenda uhalifu.
Ameongeza kuwa jeshi hilo linaendelea kuwahoji na mara baada ya upelelezi kukamilika, hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.