Kamishina wa Bima Dkt.Saqware Baghayo akizungumza kuhusiana na mafanikio ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bimq Nchini (TIRA) katika kipindi cha awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imesema kuwa katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Mali na Mitaji Katika Soko la Bima thamani imeongezeka kutoka shilingi trilioni 1.277 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi trilioni 2.340 mwaka 2024, sawa na jumla ya ongezeko la asilimia 83.3.
Wastani wa ongezeko la asilimia 16.3 kwa mwaka na kwa kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2025 (Januari – Juni) thamani ya mali katika soko la bima iliongezeka kutoka shilingi trilioni 2.340 mwishoni mwa mwaka 2024 hadi kufikia shilingi trilioni 2.495 kufikia tarehe 30 Juni 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.6.
Hayo ameseyama Kamishina wa Bima Dkt.Seqware Baghayo wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari katika Mkutano ulioratubiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo kuzungumza kuhusiana mafanikio.
Dkt.Bghayo amesema mafanikio Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya bima nchini.
Amesema kupitia sera madhubuti na mazingira wezeshi ya uwekezaji, sekta hii muhimu kwa ustawi wa jamii na uchumi wa taifa imeendelea kukua kwa kasi, kuongeza upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi, na kuongeza uwezo wa kukabili majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri maisha na uchumi wa nchi.
Aidha amesema Watanzania wengi zaidi sasa wananufaika na huduma za bima, huku fidia zikitolewa kwa walioathirika na majanga mbalimbali, hivyo kusaidia kulinda maisha na mali zao.
Dkt. Baghyo amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi mahususi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuweka mikakati na kuchukua hatua mbalimbali za kisera, kisheria na kiutendaji kuimarisha sekta hii.
Serikali ya Awamu ya Sita katika Sekta ya Bima katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetekeleza mambo mengi muhimu ambayo yamewezesha ukuaji na uimarishaji wa sekta ya bima nchini. Hatua hizo zilizochukuliwa na Serikali zimeongeza upatikanaji wa huduma bora za bima kwa wananchi, kuvutia wawekezaji wapya, na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa Sekta ya Bima .
Dkt.Baghayo amesema Serikali, kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi, imeendelea kuratibu na kushiriki kwenye matamasha ya kibiashara ya bima ndani na nje ya nchi katika kuhamasisha Umma kuhusu dhana na umuhimu wa bima, kujenga mahusiano ya kibiashara, na kufungua fursa mpya za uwekezaji katika Sekta ya Bima.
Amesema Wawekezaji wapya wamevutiwa na mazingira bora ya ufanyaji wa biashara ya bima na uthabiti wa kiuchumi.
Amesema Kutungwa kwa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote na Kanuni zake ni miongoni mwa mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kutungwa kwa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote mwaka 2023 na Kanuni zake. Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais, ikiwa ni hatua ya kihistoria inayolenga kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma bora za afya kupitia mfumo wa bima.
Aidha, mwaka 2024, Serikali kupitia Wizara ya Afya iliandaa na kupitisha Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote ili kuwezesha utekelezaji wa Sheria hiyo muhimu. Kanuni hizo zimeweka misingi ya utekelezaji, usimamizi, na ushirikishwaji wa wadau katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya bima ya afya kwa kila Mtanzania.
Aidha, Serikali imendelea kuhakikisha kuwa miradi yake mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini, ikiwemo ya miundombinu, inakuwa na kinga ya bima kutoka kwa kampuni za bima za ndani ili kulinda mali na uwekezaji unaofanywa na Serikali.
Amesema hatua hiyo inalinda uwekezaji wa Taifa na kuhakikisha kuna uendelevu wa miradi hiyo muhimu kuanzishwa kwa Konsortia ya Bima ya Kilimo kupitia ushirikiano na wadau, Serikali imeanzisha Konsotia ya Bima ya Kilimo kwa lengo la kuwahudumia wakulima, kupunguza athari za majanga ya asili, na kuongeza tija katika sekta ya kilimo pamoja na kuanzishwa kwa Konsotia ya mafuta na gesi: Sekta ya mafuta na gesi, ikiwa ni eneo la kimkakati kwa uchumi wa nchi, imenufaika na uanzishwaji wa konsotia maalum ya bima inayolenga kusimamia hatari na kulinda uwekezaji katika maeneo haya muhimu kwa uchumi wa nchi.
Amesema kuwa TIRA imefanikisha hatua kubwa ya kuunganisha mifumo ya TEHAMA ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na taasisi nyingine muhimu za Serikali. Miongoni mwa taasisi zilizounganishwa ni pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mamlaka ya Usafiri Baharini (TASAC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), na taasisi nyinginezo na muunganiko huu wa mifumo umesaidia kuongeza uwazi, ufanisi wa usimamizi wa taarifa, urahisi wa kufuatilia mwenendo wa sekta ya bima, na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Hatua hii ni ya kimkakati katika kujenga sekta ya bima inayozingatia matumizi ya teknolojia na inayoshirikiana kikamilifu na mifumo mingine ya kitaifa kwa maendeleo endelevu.
Kuimarisha matumizi ya kidijitali: Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka mazingira wezeshi yanayochochea matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa Umma. Kupitia mazingira ya biashara yaliyoboreshwa, (TIRA) imetengeneza mfumo wa kidijitali wa usajili unaowawezesha wananchi na wawekezaji wanaotaka kutoa huduma za bima nchini kuweza kujisajili mahali popote walipo na
kupitia mfumo huo, waombaji wa usajili hawalazimiki kufika katika ofisi za TIRA, bali wanaweza kutuma maombi yao mtandaoni, kufuatilia hatua kwa hatua, na hatimaye kupata cheti cha usajili kwa njia ya kidijitali. Hatua hii imeongeza uwazi, kuondoa urasimu, kupunguza gharama na muda wa usajili, na kuimarisha utoaji wa huduma kwa kasi na ubora unaotarajiwa katika zama za kidijitali.
Amesema watoa huduma za bima Idadi ya watoa huduma za bima imeongezeka kutoka 993 mwaka 2021 hadi kufikia 2,425 Juni 2025, sawa na ongezeko la jumla la asilimia 144.2. Ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 22.1 kwa mwaka. Aidha, katika kipindi hicho, Mamlaka imeongeza aina mpya ya watoa huduma ikiwa ni pamoja na watoa huduma za afya (HSPs), warekebishaji na watengenezaji magari (ARMs) na Watoa Huduma Kidijitali. Vilevile, kampuni za bima mtawanyo nchini zimeongezeka kutoka kampuni moja (1) mwaka 2021 hadi kampuni nne (4) mwaka 2025;
Dkt.Baghayo amesema usajili wa watoa huduma za bima hadi kufikia tarehe 30 Juni 2025 Watoa huduma 2021 30 Juni 2025 Kampuni za Bima Mtawanyo Kampuni za Bima 32 hadi kufiki 35 Skimu za Bima ya Afya ya Umma , Washauri wa Bima 82 hadi 146 Mawakala wa Bima 789 1,419 Washauri wa Bima Mtawanyo 4 11 Benki wakala 23 hadi 35 Kampuni za Takwimu B Wakadiriaji Hasara 50 hadi 68 Wauza Bima Kidijitali 17,kampuni ya Usimamizi wa Amana na Mifuko ya Pensheni Maafisa wauza bima (SFEs) 280,Watoa huduma za afya (HSPs) 154 ,Watengenezaji na watunza magari (ARMs) 239 Wakaguzi wa nje wanaohuduma sekta ya 993 hadi kufikia 2,425.
Wanufaika wa Huduma za Bima Wanufaika wa huduma za bima nchini wameongezeka kutoka milioni 14.2 mwaka 2021 hadi kufikia milioni 25.9 mwaka 2024, sawa na jumla ya ongezeko la asilimia 82.4 katika kipindi cha miaka minne, ikiwa ni wastani wa ongezeko la asilimia 22.2 kwa mwaka huku ajira rasmi katika soko la bima zimeongeze kutoka wafanyakazi 3,527 mwaka 2021 hadi kufikia wafanyakazi 6,916 tarehe 30 Juni 2025 sawa na ongezeko la asilimia 96.1.
Aidha, thamani ya mitaji katika soko la bima imeimarika kutoka shilingi bilioni 416.0 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi bilioni 847.3 mwaka 2024, sawa na jumla ya ongezeko la asilimia 103.7, ikiwa ni wastani wa ongezeko la asilimia 26.3 kwa mwaka. Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025, thamani ya mitaji katika soko la bima iliongezeka kutoka shilingi bilioni 906 mwaka 2024 hadi bilioni 993 kufikia Juni 30, 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.5; 4.5 Uandikishaji wa ada za bima
Uandikishaji wa ada za bima katika soko la bima nchini umeongezeka kutoka shilingi bilioni 911.5 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi trilioni 1.418 mwaka 2024, sawa na jumla ya ongezeko la asilimia 55.6 katika kipindi cha miaka minne, ikiwa ni wastani wa ongezeko la asilimia 11.7 kwa mwaka. Aidha, katika kipindi cha Januari hadi Juni 2025, uandikishaji wa ada za bima umefikia shilingi bilioni 831.8.