…………
Na WMJJWM- Dar Es Salaam
Wadau mbalimbali wa mawndeleo wamehimizwa kuunganisha nguvu katika utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029 ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Hayo yamesemwa mkoani Dar Es Salaam Agosti 18, 2025 na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu.
wakati wa akifungua Kongamano kuelekea Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029.
Dkt. Jingu amesema ni muhimu kuimarisha elimu na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa usawa wa kijinsia kama msingi wa amani endelevu, sambamba na kuweka mifumo thabiti ya ufuatiliaji na tathmini ili kuhakikisha kuwa hatua zinazochukuliwa zinafanikiwa na zinaendana na malengo ya Mpango Kazi huo.
“Kwa kufuata mwelekeo huu, Tanzania itaendelea kujenga hadhi yake kama mfano wa kuigwa, ikithibitisha kuwa ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama si ndoto bali ni hatua halisi za maendeleo, usawa na ustawi wa kijamii.” amesema Dkt. Jingu
Kwa upande wake Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UN Women Katherine Gifford, amesema Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029 ni mwelekeo mzuri katika kuhakikisha Mwanamke anashirikishwa katika masuala ya amani na usalama hivyo Mpango huo unapaswa kuwekwa katika utekelezaji zaidi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Brigedia Jenerali George Itang’are ameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kuandaa Mpango Kazi huo ambao ni mwanzo wa mabadiliko makubwa ya kuhakikisha Mwanamke anashirikishwa katika masuala muhimu ya amani na usalama.