Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amewataka Wananchi kuunga Mkono miradi inayoanzishwa na Serikali ili iweze kukamilika kwa muda uliopangwa.
Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati alipofanya ziara ya kukaguwa maeneo yanayotarajiwa kujengwa Viwanja vya Mpira wa Miguu hapa Nchini.
Amesema Serikali inatumia Fedha nyingi kuendesha miradi ya Michezo kwa Wananchi hivyo ni vyema kutoa maeneo wakati Serikali inapoyahitaji.
Aidha amesema Serikali itaendelea kuimarisha Miundombinu ya Michezo kwa maslahi ya Wanamichezo na Taifa kwa Ujumla.
Hata hivyo amewataka Masheha na Wakuu wa Wilaya, zinazotarajiwa kujengwa Viwanja hivyo kutoa elimu kwa Wananchi ili Ujenzi huo, uweze kufanyika kwa Ufanisi.
Kwa Upande wake Kanishna Idara ya Michezo Zanzibar Ameir Mohammed Makame amesema lengo la ziara hiyo ni kukaguwa maeneo hayo na kuangalia Changamoto mbalimbali zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
Sambamba na hayo amewataka Wananchi kushirikiana na Serikali wakati miradi itakapoanza ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
Mhe. Tabia amefanya ziara katika maeneo mbalimbali yanayotarajiwa kujengwa viwanja vya Wilaya ya Mikoa ikiwemo Kijini Matemwe, Pwani Mchangani, Kama na Mtoni, eneo ambalo linapotarajiwa kujengwa kiwanja cha Mpira wa Ufukweni.