Na Issa Mwadangala.
Elimu hiyo ilitolewa Agosti 19, 2025 na Polisi kata ya Nambino Mkaguzi wa Polisi, Issa Mudu, akitoa elimu kwa wana michezo hao juu ya athari mbalimbali za ukatili wa kijinsia katika familia hasa wanawake na watoto, jamii na taifa kwa ujumla.
Mkaguzi Mudu akizungumza mbele ya wachezaji na mashabiki waliohudhuria, alisisitiza kuwa ukatili wa kijinsia siyo tu kosa la jinai, bali pia ni chanzo cha kuvunjika amani ikiwa ni Pamoja na misingi ya upendo, heshima na mshikamano katika jamii.
“Ukatili wa kijinsia unaweza kusababisha majeraha ya kimwili na kisaikolojia, kuporomoka kwa maendeleo ya watoto shuleni, kuenea kwa magonjwa ya zinaa, pamoja na kuongezeka kwa vifo vitokanavyo na unyanyasaji wa kijinsia” alisema Mkaguzi Mudu.
Vilevile, Mkaguzi Mudu aliwahimiza wachezaji na wadau wa michezo kuwa na ushirikiano na jamii, viongozi wa dini, walimu na wazazi katika kutoa elimu ya maadili na kuripoti matukio ya ukatili, pia aliwahimiza vijana kuepukana ya matumizi ya dawa za kulevya na kuzingatia nidhamu katika maisha yao kwa manufaa ya maendeleo kila siku.
Aidha, Mkaguzi Mudu aliwasisitiza kuwa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia si wa Jeshi la Polisi tu bali ni jukumu la kila mmoja, na kwamba kila mwanajamii anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake kwa kuhakikisha hakuna anayefanyiwa ukatili kimya kimya bila kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa haraka.

