Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa Agosti 22, 2025 amemkabidhi boti moja mpya PB.44 ULINZI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga.
Akikabidhi boti hiyo kwa Jeshi Mkoa wa Mbeya, Mhe Malisa amelitaka Jeshi hilo kulitumia vizuri boti hilo katika kuimarisha doria za ziwa nyasa Wilayani Kyela na kutokomeza uhalifu.
Aidha, Mhe.Malisa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa kutimiza ahadi ya kutoa boti kwa ajili ya kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa na kuahidi kuitunza na kuitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa.
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema kuwa Boti hiyo inakwenda kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa kupitia doria za pamoja za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Ziwa nyasa ni miongoni mwa maziwa makuu nchini ambalo sehemu ya Ziwa hilo ni nchi jirani ya Malawi na Mkoa wa Njombe na Ruvuma hivyo uwepo wa Boti hiyo ni mikakati ya kuimarisha ulinzi na kudhibiti uhalifu wa majini, JWTZ, Uhamiaji na TRA.