Baada ya uteuzi wa wagombe ubunge wa uliofanyika siku ya Jana na halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa, Mbunge wa Jimbo la Ludewa Adv. Joseph Zacharius Kamonga Leo majira ya saa 9 Alasiri ametinga ofisi za Tume ya uchaguzi wa Jimbo hilo na kuchukua fomu tayari kwa kuipeperusha bendera ya CCM.
Kamonga ameingia Tena katika kinyang’anyiro hicho baada ya kumaliza kipindi chake Cha uongozi kwa miaka mitano 2020/2025.