Kutoka kushoto ni Mgombea wa nafasi ya Ubunge Silvestry Koka akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mwalimu Mwajuma Nyamka.
Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MBUNGE Mteule wa Jimbo la Kibaha Mjini Mhe.Silvestry Koka anetoa rai kwa wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kuchagua Mbunge na Madiwani wa CCM.
Pia amesema kuanzia sasa ndiyo muda muafaka wa kusafishana nyoyo na kwenda kusaka ushidi wa kishindo kwa CCM.
“Sisi tunarekodi nzuri ya msingi mzuri na imara na tuliujenga kwenye kuajiandikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na tulishinda kwa kishindo,hatuna uoga wa kushinda na namba yetu ikabaki palepale namba moja.
Koka amesema hayo leo tarehe 24 Agosti 2025 alipozungumza kwenye mkutano na wanachama na wananchi wa Kibaha Mjini kwenye mkutano uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Wilaya CCM Kibaha Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kibaha Mwalimu Nyamka amesema kuwa anawasisitiza kwamba Mbunge Koka na Madiwani wote wa Kata 14 wanapata kura za kutosha .
“Twendeni tukazitafute kura za Chama Cha Mapinduzi CCM ni imani yangu kwamba kwa mkudanyiko huu tunasubiri kuthibitishwa,
Kipekee nimefurahishwa kuwaona wagombea ambao walitia nia na Mgombea wako hapa tumetembea nao nawapongeza na nawashukuru sana wameturahisishia kazi ta kwenda kurafuta kura za CCM,wamemwaga mambo hadharani kwamba Chama kwanza mtu baadaye”amesema Mwalimu Nyamka.
Chama kimeshatuletea wagombea wewe nani bado unabaki na vinyongo twendeni tukavunje makundi na makundi yanavyunjwa na walioshinda kaacheni majigambo ambayo yatawapa wengine unyonge, wakati wa mchakato mambo mengi yamepita lakini lengo lao wote walikua wanatafuta nafasi yaliyopita si ndwele tugange yajayo” amesema Nyamka.
“Kuanzia leo mkikuta kuna mtu anaendeleza kumchafua mtu huku na yeye ni mwanachama basi mjue huyo hayuko sawa”amesema Nyamka.
Akizungumza aliyekua mtia nia Aljaji Mussa Mansuri amesema katika uchaguzi huo watia nia na mgombea wamefanya mazoezi, tunawapongeza wagombea wote waliopita.
“Koka ni Jemedari wa Jimbo la Kibaha Mjini hivyo nawaomba ndugu zangu nguvu zote tuhakikishe tunaelekeza katika kukipigania Chama Cha Mapinduzi
( CCM) ,naahidi ndani ya moyo wangu wewe ndiyo dira yetu na wewe ndiyo wa kutuunganisha na unatakiwa uwe Kiongozi mlezi” amesema Mansuri.
Mhe.Koka amesema kuwa Madiwani wengine watachaguliwa kutoka Mbawa ,Visiga ,Misugusugu, Kongowe ,Viziwaziwa ,Mkuza ,
Kibaha ,Msangani ,Pangani, Tangini ,Mailimoja ,Picha ya Ndege, Tumbi na Sofu.
Koka anatarajiwa kurudisha fomu hiyo tarehe 27 Agosti 2025 ambapo atakua tayari kwa kuanza kampeni za uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika tarehe 29,Oktoba 2025