
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema haitafuata maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo yamebatilisha uteuzi wa Luhaga Mpina kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
Kwa mujibu wa chama hicho, Msajili hana mamlaka ya kuingilia mchakato wa kuteuliwa mgombea wa urais isipokuwa kupitia hatua ya pingamizi, na hatua ya kutengua uteuzi huo haiwezi kutumika moja kwa moja.
ACT-Wazalendo imesema itachukua hatua ya kisheria kwa kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo na kuweka zuio dhidi ya utekelezwaji wa uamuzi wa Msajili.