Dar es Salaam, Agosti 28, 2025 – Airtel Money Tanzania leo
imetangaza uzinduzi wa kampeni mbili kabambe maalum kwa wateja wake wa Airtel
Money itakayojulikana kama Airtel Money Ni Buree na Ni Nafuu, ikiwa na lengo la
kuendelea kutoa uhuru zaidi kwa wateja wote wanaotumia Airtel Money.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Makao
Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Airtel Money,
Andrew Rugamba, alisisitiza manufaa ya kampeni ya Airtel Money ni Bure na Ni
Nafuu:
“Kampeni Airtel Money ni Bure na Ni Nafuu inaleta unafuu
zaidi katika kutuma na kutoa pesa, ikiwasaidia wateja wetu kuokoa zaidi na
kuwapa uhuru wa kufanya mambo mengi zaidi kwa fedha zao.
Airtel Money Ni Bure, mteja ataweza kufanya miamala yake ya
kutuma pesa Airtel Kwenda Airtel BURE kupitia my Airtel APP kiwango cha hadi
milioni 5,
Airtel Money Ni Nafuuu, mteja wetu ataweza kutoa pesa chini
ya kiwango cha shilingi 10,000 BURE Bila TOZO ya serikali. Hii inamaana ya kwamba Airtel tutalipa TOZO
hiyo ili mteja wetu aweze kufanya muamala wake BURE kabisa.
Uzinduzi huu unathibitisha dhamira ya Airtel kuunga mkono
juhudi za Serikali za kukuza ujumuishi wa kifedha kupitia mifumo ya kidijitali
na kuharakisha safari ya kuelekea kwenye uchumi usiotegemea pesa taslimu.
Airtel Money tunaamini
huduma za kifedha zinapaswa kuwa nafuu, jumuishi na kupatikana kwa kila
mmoja. Airtel Money kwa kuamua kubeba gharama za huduma za kutoa pesa chini ya shilingi elfu
kumi, au kuwezesha Wateja wetu kutuma pesa Kiwango chochote BURE kupitia App yetu, tunajibu moja kwa moja mahitaji ya
huduma bora na nafuu ambapo-hii itasaidia wateja wetu kuokoa pesa na kuzitumia
kufanya mambo mengine iwe ni kununua umeme, muda wa maongezi au huduma nyingine.
Hivi ndivyo tunavyosukuma mbele ujumuishi wa kifedha na kufanya miamala ya
kidijitali kuwa nafuu kwa kila Mtanzania.”
Rugamba aliongeza kuwa kampeni za Airtel Money Ni Buree na
Ni Nafuu zimetengenezwa ili kuimarisha mfumo wa kifedha wa kidijitali nchini na
kuongeza manufaa kwa wateja katika kila muamala wanaofanya.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Airtel jackson Mmbando
alisema: “Wateja wetu wametuambia wanataka huduma nafuu zaidi na rahisi zaidi.
Airtel Money Ni Nafuu inaleta yote mawili. Airtel Money Ni Bureee na
Nafuuu inathibitisha dhamira ya Airtel
katika kutoa huduma za kifedha zilizo nafuu, bunifu na jumuishi ambazo
zinaendana na dira ya kitaifa ya Tanzania ya kuwa na uchumi imara wa
kidijitali.”